1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa usafiri wa Umoja wa Ulaya wafanya mkutano

Kabogo Grace Patricia20 Aprili 2010

Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video ulikuwa ukitathmini marufuku ya safari za ndege iliyosababishwa na wingu la majivu yaliyotokana na kuripuka volkano nchini Iceland.

https://p.dw.com/p/N0iD
Abiria wakiwa kwenye uwanja wa ndege wanasubiri safari zao.Picha: AP

Mawaziri wa usafiri wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kufungua sehemu ya anga iliyokuwa imefungwa kutokana na wingu la majivu yaliyosababishwa na mripuko wa volkano nchini Iceland.

Hatua hiyo imefikiwa katika mkutano wao wa dharura walioufanya jana kwa njia ya video. Waziri wa Usafiri wa Ujerumani, Peter Ramsauer alisema kuwa ndege zitaanza kurejea katika hali ya kawaida kuanzia leo, ingawa itakuwa kulingana tu na masharti makali ya usalama.

Maelfu ya wasafiri wameendelea kukwama kufuatia kufungwa kwa anga za maeneo mengi ya Ulaya kwa siku ya tano mfululizo. Mashirika ya ndege yamesema yamepata hasara ya zaidi ya euro milioni 740. Anga ya Ujerumani itaendelea kufungwa hadi angalau mchana wa leo.