1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

May akiri makubaliano ya Brexit hayatapita bungeni

Iddi Ssessanga
7 Aprili 2019

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekiri kuwa mikakati ya serikali kuidhishwa mpango wake wa Brexit bungeni imefeli, akisema kuna matarajio madogo kwa wabunge kuunga mkono makubaliano yaliokataliwa mara tatu.

https://p.dw.com/p/3GPlF
Brexit - Britische Premierministerin May
Picha: picture-alliance/dpa/G. V. Wijngaert

Huku Uingereza kwa mara nyingine ikibakisha siku chache tu kutoka tarehe ya mwisho ya kuondoka Umoja wa Ulaya, May aliwashinikiza wabunge wa upinzani kusaidia kupatikana kwa makubaliano ya muafaka, akisema wapigakura "wanatarajia wanasiasa wao kushirikiana pale maslahi ya kitaifa yanapotaka hivyo."

Baada ya makubaliano ya May na Umoja wa Ulaya kukataliwa kwa mara ya tatu na bunge, waziri mkuu huyo alikialika chama cha upinzani cha Labour wiki hii kujadili mikakati mbadala. Lakini siku tatu za mazungumzo ziliisha bila makubaliano na chama hicho cha Labour kikiishtumu serikali ya kihafidhina ya May kwa kutotoa mabadiliko ya kweli.

"Sijaona mabadiliko yoyote makubwa katika msimamo wa serikali mpaka sasa," alisema kiongozi wa Labour Jeremy Corbyn siku ya Jumamosi. "Nasubiri kuona misitari miekundu ikihamishwa."

Chama cha Labour kinapendelea mchakato laini wa Brexit kuliko ilivyopendekezwa na serikali. Chama hicho kinasema Uingereza inapaswa kubakia ikiongozwa na sheria za Umoja wa Ulaya kuhusu biashara na kuendeleza viwango vya kanda hiyo katika maeneo kama haki za wafanyakazi na ulinzi wa mazingira.

London - Großbritannien - Jeremy Corbyn - Labour Parteichef
Kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn amesema hajaona mabadiliko katika msimamo wa serikali ya kihafidhina ya waziri mkuu Theresa May.Picha: Getty Images/AFP/D. Leal-Olivas

May aomba kuondoka Juni 30

Uingereza inatarajiwa kuondoka Umoja wa Ulaya siku ya Ijumaa iwapo May hatopata makubaliano ya kurefusha tena mchakato kutoka Umoja wa Ulaya, ambao tayari ulikubali kurefusha siku ya Brexit iliyopangwa awali kuwa Machi 29. May sasa anaomba muda wa kuondoka Uingerea urefushwe hadi Juni 30, akitumai kufikia muafaka na chama cha Labour na makubaliano kupitishwa na bunge katika muda wa wiki chache.

"Kadiri hii inavyochukuwa muda mrefu, ndiyvyo hatari inavyoongezeka ya UK kuoondoka kabisaa," alisema May katika taarifa. Lakini Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanapendelea ucheleweshaji mrefu zaidi ili kuepusha duru nyingine ya  matatizo ya maandalizi na kisiasa. Na wanasema Uingereza inahitaji kuwasilisha mpango madhubuti wa kukomesha mkwamo ili kupata uahirishaji zaidi.

Urefushaji unahitaji idhini ya viongozi wa mataifa yote 27 wanachama yanayosalia, ambao baadhi yao wamechoshwa na mashaka ya Brexit na wanasita kurefusha zaidi mchakato huo.

Mwezi uliopita, Umoja wa Ulaya uliipa Uingereza hadi Aprili 12 kuidhinisha makubaliano ya kujiondoa uliofikia na serikali ya May, kubadili mkondo na kutafuta ucheleweshaji zaidi wa Brexit, au kuondoka bila makubaliano au kuwepo na kipindi cha mpito kupunguza mshtuko.

Infografik Deutschlandtrend Brexit EN
Uchunguzi wa taasis ya Infratest dimap unaonyesha kuwa idadi kubwa zaidi ya Waingereza wanajutia Brexit-

Ireland yasema atakaezuwia kurefusha muda hawatomsamehe

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana mjini Brussels siku ya Jumatano - siku mbili kabla ya tarehe ya mwisho ya Aprili 12 - kuzingatia ombi la Uingereza kuhusu urefiúshaji wa pili.

Wachumi na viongozi wa kibishara wameonya kuwa Brexit bila makubaliano itavutuga vibaya biashara na usafiri, ambapo kodi na ukaguzi wa forodha vinaweza kusababisha msongamano kwenye bandari za Uingereza na uwezekano wa kutokea uhaba wa baadhi ya vyakula, dawa na biadhaa nyengine.

Wasiwasi wa Brexit ya vurugu ni mkubw ahasa nchini Ireland, nchi pekee ya Umoja wa Ulaya inayoshiriki mpaka na Uingereza. Kurejea kwa ukaguzi wowote wa mpakani au vikwazo vingine kwenye mpaka wa sasa usioonekana kutaathiri uchumi wa Ireland na kudhoofisha mchakato wa amani wa Ireland ya Kaskazini.

Waziri Mkuu wa Ireland Leo Varadkar alisema siku ya Jumamosi kwamba "kuna uwezekano mdogo sana" kwamba yeyote kati ya viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya atazuwia ucheleweshaji.

"Iwapo nchi moja ingezuwia urefushaji na, kama matokeo, ikatuwekea ugumu sisi, matatizo halisi kwa Waholanzi, Wafaransa na Wabelgiji kama majirani wa Uingereza...hawangesamehewa kwa hatua hiyo," alikiambia kituo cha redio cha Ireland RTE.

vyanzo:ape,afpe