1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazishi ya polisi watatu wa Ujerumani waliouliwa Afghanistan yanafanyika leo mjini Berlin

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBY4

Berlin:

Ibada rasmi ya mazishi ya askari polisi watatu wa kijerumani waliouliwa hivi karibuni nchini Afghanistan,inafanyika hii leo katika kanisa kuu la mjini Berlin.Askari polisi hao waliuliwa jumatano iliyopita gari waliyokua wakisafiria iliporipuliwa nchini Afghanistan.Kansela Angela Merkel na waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble watahudhuria ibada hiyo.Kabla ya hapo kumbu kumbu za mazishi zitafanyika katika uwanja wa ndege wa Tegel mjini Berlin, wakihudhuria familia za wahanga hao tuu.Ndege ya jeshi la shirikisho Bundeswehr ikisafirisha maiti za polisi hao watatu inatazamiwa kutuwa leo mchana katika uwanja wa ndege wa Tegel.Waziri mkuu wa jimbo la kusini la Bavaria Edmund Stoiber amepinga fikra ya kutumwa wanajeshi zaidi wa Ujerumani nchini Afghanistan.Hoja zake zimekosolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje Gernot Erler na waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer.