1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo baina ya Iran na Marekani.

17 Mei 2007

Viongozi wa Iran na Marekani watafanya mazungumzo juu ya hali kisiasa nchini Iraq wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/CHEA

Kwa mara ya kwanza waku wa serakali ya Iran na serakali ya Marekani watakutana ana kwa ana, tare 28 mwezi huu wa May mjini Baghdad.

Haya yatakua mazungumzo ya kwanza, nchi mbili hizi kukutana tangu mapinduzi yaliofanywa na wazee wa kidini nchini Iran, kumuondoa Mfalme Shah madarakani mwaka 1979.

Waziri wa mambo ya njee wa Iran Bw Manouchehr Mottaki alitangaza habari hio akiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za njee wa nchi za kiislamu mjini Islamabad pakistan.

Bw Mottaki alisisitiza kua mazungumzo hayo yatahusu ttu, kutafuta njia za kumaliza machafuko nchini Iraq na sio suala lolote jengine.

Licha ya Iran na Marekani kutokua na uhusiano wa kibalozi , lakini nchi mbili hizi zitawakilishwa na maafisa wa ngazi za kibalozi, wakiwepo pia waku wa Iraq katika mazungumzo haya yatakayo fanyika mjini Baghdad.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Tony Snow, amesema mkutano huu wa Baghdad hautobadilisha msimamo wa Marekani kuitenga Iran,

kwa kuyasaidia makundi ya wanamgambo waki shiia yanayo hujumu vikosi vya ki Marekani, huku Marekani ikizidi pia kuilaumu Iran kwamba, inatengeneza mtambo wa silaha za ki Nuclear .

Lakini waziri Mottaki alisema , la msingi Marekani sasa inafahamu kua, sera yake ya kuitawala Iraq imefeli, tangu kuivamia nchi hio mwaka 2003.

Alisema Iraq inakabiliwa na hali mbaya ya usalama inayosababishwa na visa vya kigaidi, na pia, nchi hio kuendelea kukaliwa kimabavu .

Waziri Mottaki alisema tangu mwezi March mwaka jana, Iran ilivunja mazungumzo yaliokua yakiendelea na Marekani, kutafuta Amani nchini Iraq , kutokana na propaganda nyingi za Marekani dhidi ya Iran

Kiongozi mku wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, alisema, hatarajii mazungumzo haya na Marekani kuleta tiija yoyote, lakini itakua uzuri kuikumbusha Marekani sio jukumu lao Marekani, kuikalia nchi hio ya Iraq.

Hapo awali wanasiasa wa Iran wenye mrengo wa kihafidhina, waliwalaumu waku wa Iran kukubali kufanya mazungumzo na Marekani, na kusema kua kitendo hicho , ni sawa na kucheza na mbwa mwiitu au kusalimiana na shetani kwa kupeana mikono.