1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kuhusu Kosovo yameshindwa

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUcb

New-York:

Umoja wa mataifa umetoa mwito wa kuendelezwa juhudi za upatanishi hata baada ya kushindwa duru mpya ya mazungumzo kuhusu mustakbal wa Kosovo jana mjini Vienna.Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ban Ki-Moon anasema hata kama mazungumzo ni tete,lakini anaamini maridhiano yanaweza kufikiwa.Wawakilishi wa pande tatu zinazosimamia mazungumzo hayo,Umoja wa Ulaya,Marekani na Urusi wametakiwa waendelee na juhudi zao kusaka ufumbuzi hadi December 10 ijayo.

Wakosovo wenye asili ya Albania wanadai uhuru wa jimbo hilo linalosimamiwa na jumuia ya kimataifa.Wa Serbia lakini wanasema wako tayari kuwapatia utawaa mkubwa tuu wa ndani.