Mazungumzo nyeti kati ya Israel na Wapalestina kuanza leo
14 Januari 2008Matangazo
JERUSALEM
Wasuluhishi waandamizi wa Israel na Palestina leo wanatazamiwa kuanza mazungumzo kama sehemu ya shinikizo la Marekani la kufikiwa kwa makubaliano ya amani kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
Rais Mahamoud Abbas wa Wapalestina amesema msuluhishi wake mkuu Ahmed Qorei na waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni wataongoza mazungumzo hayo juu ya masuala muhimu ambayo wanataraji yatapelekea kuundwa kwa taifa huru la Wapalestina.
Masuala hayo yanajumuisha mustakbali wa mji wa Jerusalem, uchoraji wa mipaka na hatima ya wakimbizi wa Kipalestina.