1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Bali hatarini kukwama

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbBa

NUSA DUA,Indonesia

Mkuu wa masuala ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba kukwama kufikia makubaliano kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya juu ya viwango vya kudhibiti utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira duniani kunatishia kuvuruga mazungumzo yenye lengo la kuzinduwa mazunmguzo kwa ajili ya mkataba mpya wa kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Ikiwa karibu zinafikia wiki mbili mazunngumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakiingia mkondo wa mwisho Yvo de Boer amesema ana wasi wasi kwamba iwapo nchi moja haitokubali viwango hivyo vya kudhibiti utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira mchakato huo mzima utakuwa ni kazi ya bure.

Serikali ya Marekani imegoma lugha iliotumiwa kwenye rasimu ya waraka inayodokeza kwamba mazungumzo yajayo kwa ajili ya mkataba wa kuchukuwa nafasi ya Itifaki ya Kyoto iziombe nchi tajiri zenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani kufikiria utowaji wa gesi hizo kwa kiwango cha asilimia 25 hadi asilimia 40 ifikapo mwaka 2020.

Umoja wa Ulaya unapendelea uwekaji wa maudhui yanayotaja viwango mahsusi.