1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kuunda serikali yaingia hatua za mwisho

Sekione Kitojo
4 Februari 2018

Wahafidhina wanaoongozwa na kansela Merkel watakaa pamoja na hasimu wao wa kihistoria chama cha SPD Jumapili (04.02.2018) kujaribu kufikia makubaliano ya kuunda serikali zaidi ya miezi minne baada ya uchaguzi wa bunge.

https://p.dw.com/p/2s5rs
Kombobild Koalitionsverhandlungen- Martin Schulz und Angela Merkel

Wamejiwekea muda  wa  mwisho kuwa  leo  Jumapili jioni (04.02.2018), wakiwa  na  fursa ya  kurefusha  mkutano  wao  hadi Jumatatu  ama  Jumanne. Katika  ajenda  ni  maswali yaliyoainisha  vyema  juu  ya  vipi marudio  ya  kile  kinachofahamika  kama  "Muungano Mkuu"  ama  kama  unavyofahamika  nchini  kwa  Kijerumani "GroKo" ambao  umekuwa madarakani  tangu  mwaka  2013 utaelekeza  huduma  za  afya, sheria  za  kazi, malipo ya uzeeni  na  mageuzi  ya  Umoja  wa  Ulaya  na  sarafu  ya  pamoja  ya  euro.

Deutschland Koalitionsverhandlungen von Union und SPD
Mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano Andrea Nahles (katikati) akiwasili kwa ajili ya majadilianoPicha: Reuters/C. Mang

Pande zote  mbili zinasita  kufikia maridhiano  ya  kupita  kiasi  na  kuhatarisha  kupoteza uungwaji  mkono, lakini  pamoja  na  hayo  pande  hizo  zina  hofu ya  kurejea  kwa  wapiga kura  katika  uchaguzi  wa  marudio ambao unaweza  kushuhudia  kupanda  juu  zaidi  kwa kundi  la  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia.

Lakini  pia  hakuna  upande  unaweza  kung'ang'ania  msimamo  wake , wakati  utafiti  wa maoni  uliofanywa  kwa  niaba  ya  kituo  cha  televisheni  ya  taifa  cha  ARD unaonesha asilimia  721 ya  watu  hawaelewi "kwanini  uundaji  wa  serikali  unachukua muda  mrefu hivyo".

"Nina matumaini tunaweza  kutimiza," Merkel  amesema  Ijumaa, akionya  hata  hivyo kwamba  bado  kuna  "orodha  nzima ya  vipengee  muhimu  ambavyo  bado hawajakubaliana".

Deutschland Merkel, Seehofer und Gabriel ARCHIV
Viongozi wa majadiliano ya kuunda serikali Horst Seehoffer (kushoto)kansela Merkel (katikati ) na kiongozi wa SPD Martin Schulz (kulia)Picha: picture alliance/dpa/M. Gambarini

Serikali imara

Cha  muhimu  kwa  Merkel , ambaye  bado  anaonekana  kuwa "anafanya  vizuri"  ama "vizuri sana" kwa nafasi  ya  ukansela  ambapo asilimia 51  ya  watu  walioulizwa  walisema  katika uchunguzi  huo  wa  maoni , ni  iwapo anaongoza  serikali  imara  ya  muungano  katika muhula  wake  wa  nne  wa  uongozi, ama  anahatai ya  kuingia  katika  serikali  tete  isiyo  na wingi  ama  kurejea  katika  uchaguzi  mpya.

Chama  cha  SPD ni  mshirika  wa  shingo  upande, baada  ya  hapo  kabla  kuapa  kuingia katika  upinzani  baada  ya  kupata  matokeo  ya  chini  katika  historia  ya  chama  hicho  ya asilimia  20.5  katika  uchaguzi  wa  mwezi  Septemba.

Wanachama  wa  Social Democrat walikubali  kuingia  katika  mazungumzo  pale  tu kushindwa  kukubaliana  na  vyama  vidogo , chama  cha  walinzi  wa  mazingira , cha  kijani na  kile  kinachopendelea  biashara  cha  Free Democratic FDP.

Wernigerode Landesparteitag der SPD Sachsen-Anhalt Anti GroKo Button
No GroKo kampeni ya waasi katika chama cha SPD kuzuwia uundwaji wa serikali mpyaPicha: DW/S. Kinkartz

Akipata  changamoto  kutoka kwa  waasi  katika  chama  chake, kiongozi  wa  SPD Martin Schulz aliona  bora  kupata ulinzi  wa  kisiasa  kwa  kupeleka  makubaliano  ya  mwisho  ya kuunda  serikali  ya  mseto katika  kura  ambapo  wanachama  440,000 watapiga  kura kukubali  ama  kukataa.

Tawi la vijana

Kevin Kuehnert , kiongozi  wa  tawi  la  vijana  la  chama  cha  SPD , amekuwa mshika bendera  ya  upinzani  wa  makubaliano  mapya  na  Merkel.

"Aina  hii ya  siasa  ilizawadiwa  na  upungufu  wa  asilimia  14 kwa  CDU  na  SPD  kwa jumla  mwaka  jana, na  nina  shaka  mambo  yataendelea  hivi  hivi "iwapo muungano  wa serikali  utafanikiwa, alisema.

Außerordentlicher SPD-Parteitag Juso-Bundesvorsitzender Kevin Kühnert
Kiongozi wa tawi la vijana la SPD Kevin KuehnertPicha: picture alliance/dpa/K. Nietfeld

Wengine  wanaonya  SPD  iko  dhaifu  sana  kuwakabili wapiga  kura  kwa  mara  nyingine  tena  haraka, ikipata  asilimia  18 katika  baadhi  ya uchunguzi  wa  maoni  ya  wapiga  kura, kiasi  ya  pointi  chache  mbele  ya  chama  cha siasa  kali  za  mrengo wa  kulia  cha  Alternative for Germany, chama  mbadala  kwa Ujerumani AfD.

Merkel  pia  anakabiliwa  na manung'uniko  miongoni  mwa  wanachama  wake, kukiwa  na sauti  zinazopazwa za wahafidhina zikimshutumu kwa  kukipeleka  chama  chake  cha Christian Democratic Union CDU kuelekea  zaidi siasa  za  wastani , na  kutoa  fursa  kwa chama  cha  AfD.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Yusra, Buwayhid