1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya nyuklia ya Iran kuanza tena Jumanne

7 Februari 2022

Mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani juu ya kuyafufua makubaliano ya mwaka 2015 kuhusu mpango wa nyukilia wa Iran yataanza tena siku ya Jumanne baada ya kusimama kwa siku kadhaa.

https://p.dw.com/p/46dyl
Österreich | Treffen zum iranischen Atomabkommen in Wien
Picha: EU Delegation in Vienna/REUTERS

Hayo yameelezwa na Umoja wa Ulaya ambao ndio mwenyekiti wa mazungumzo hayo yanayo fanyika mjini Vienna, Austria.

Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa Vienna mnamo 2018 chini ya utawala wa Rais Donald Trump na kisha kurejesha vikwazo vikali kwa Iran.

Rais wa sasa wa  Marekani Joe Bidern ameashiria utayari wa kujiunga tena na makubaliano hayo.

Uingereza, Ufaransa, Ujeruman, Urusi na China bado zinaendelea kuwa sehemu ya makubaliano hayo na zimekuwa zikifanya juhudi za kuyaokoa.

Soma pia: Iran yaonyesha makombora yake ya masafa marefu mjini Tehran

Siku ya Ijumaa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisaini azimio la kuilegezea vikwazo Iran kwa shughuli za kiraia za mpango huo.

Iran Atomeinigung | Gemeinsame Sitzung der JCPOA-Kommission
Mkutano wa pamoja na kamati ya JCPOA.Picha: irna

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alipongeza hatua hiyo siku ya Jumamosi lakini akaongeza kuwa haitoshi.

Iran yalenga faida za kiuchumi

Naye msemaji wa wizara ya mambo ya  nje wa Iran  Saeed Khatibzadeh  amesema jumatatu kuwa nchi yake inalenga zaidi faida za kiuchumi kutoka kwenye makubaliano hayo.

"Hakujawa na hatua zozote katika muktadha huu, Marekani imeamua kuchukua hatua katika eneo la maslahi yake yenyewe wakati tunafuatilia kwa karibu hatua zozote kuelekea njia sahihi hatua hizo haziwezi kuchukuliwa kwa uzito", alisema Khatibzadeb.

Soma pia:Rais wa Iran Ebrahim Raisi aapa kisasi kwa mauaji ya jenerali Qassem Soleimani 

Wanadiplomasia kutoka nchi tatu za Umoja za Ulaya wamesema wakati mazungumzo yaliposimama baada ya mwezi  mmoja Januari 28, majadiliano yalikuwa yanafikia hatua ya mwisho na kwamba  hilo lilihitaji maamuzi ya kisiasa.

Chanzo: AP, APTN