1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Vienna kuhusu nyuklia yarefushwa

24 Novemba 2014

Mazungumzo kuhusu mradi wa kinyuklia wa Iran pamoja na mataifa matano yenye kura ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa na Ujerumani mjini Vienna Austria yamepiga hatua muhimu

https://p.dw.com/p/1DsJZ
Mawaziri wa Mambo ya nchi za nje wa Iran na wa mataifa matano yenye kura ya turufu pamoja na waziri wa Mambo ya nchi za nje wa UjerumaniPicha: ISNA

Hata hivyo mazungumzo hayo yamerufushwa. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uengereza Philipp Hammond amesema "haikuwezekana kufikia makubaliano kama ilivyopangwa hii leo" na kwamba mazungumzo hayo hivi sasa yamerefushwa hadi julai mosi mwaka 2015.

Akizungumza na maripota waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uengereza Philip Hammond amesema "maendeleo muhimu yameweza kufikiwa katika duru hii ya mwisho ya mazungumzo iliyoanza jumanne iliyopita katika mji mkuu wa Austria Vienna.Hammond ameongeza kusema kula lengo bayana la kufikia mwongozo wa makubaliano katika kipindi cha miezi mitatu ijayo na kwamba mazungumzo yataanza upya mwezi ujao.Waziri mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov amezungumzia kuhusu "maendeleo ya maana" yaliyofikiwa na kuelezea matumaini makubaliano yanaweza kupatikana.

Matumaini kama hayo yametolewa pia na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliyesema tunanukuu:"Tunataka katika kipindi cha siku na wiki zinazokuja tuendelee kujadiliana kwa shime."

Iran itajipatia dala bilioni 700 kwa mwezi

Haijulikani lakini wapi mazungumzo ya mwezi ujao yatafanyika,ameongeza kusema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uengereza aliyefichua kwamba mnamo muda huo ambao mazungumzo yataendelea Teheran itaweza kujipatia kiasi cha dala milioni 700 kwa mwezi-kutokana na kupunguzwa makali vikwazo vya kimataifa dhidi yake.

Hasan Rohani, Iranischer Präsident
Rais Hasan Rohani wa IranPicha: jamnews

"Kimsingi makubaliano ya muda yaliyotiwa saini mjini Geneva Novemba 24 mwaka jana kati ya Iran na kundi la mataifa matano yenye kura ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa na Ujerumani,ambayo yalikuwa yamalizike leo hii ndiyo yanayaorefushwa kwa miezi sabaa-duru za kibalozi kutoka nchi za magharibi zimesema.

"Mazungumzo yataendelea wiki zijazo ili kufikia makubaliano,duru za Iran zimesema mjini Vienna.

Rais Hassan Rohani wa Iran amepanga kulihutubia taifa baadae hii leo kuhusu suala la mradi wa kinuklea wa Iran-habari hizo zimtangazwa na shirika la habari la Iran -IRNA .

IAEA lasifu hatua za Iran

Wakati huo huo shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA limesema katika ripoti yake ya kila mwezi inayomulika jinsi makubaliano ya muda yanavyotekelezwa,kwamba Iran imepunguza shehena ya gesi ya urani na kwamba inachukua hatua nyengine kujiambatanisha na makubaliano ya mpito yaliyofikiwa mwaka jana pamoja na madola makuu.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/dpa/Reuters/AFP/AP

Mhariri: Mohammed Khelef