1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo yaanza tena kati ya maafisa wa Deutsche Bahn na chama cha madreva wa treni

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cf5q

Maafisa wa shirika la usafiri wa reli hapa Ujerumani, Deutsche Bahn, na chama cha madereva wa treni, GDL, wanatarajiwa kuanza tena mazungumzo kuhusu mishahara wikendi hii kufuatia juhudi za serikali kuyataka mashirika hayo yakubali kufanya mazungumzo.

Waziri wa uchukuzi wa Ujerumani, Wolfgang Tiefensee, amesema mazungumzo hayo yanaanza leo katika mahala ambapo hapakutajwa.

´Kuna kazi kubwa ya kufanya itakayoendelea wakati wa likizo kati ya siku kuu ya Krismasi na Sylvester kwa sababu mazungumzo yana utata mkubwa. Nimeridhika kwamba mazungumzo hayo yameweza kuanza kwa haraka hivyo kuna matumaini ya kufikia makubaliano.´

Chama cha madreva wa treni kilijiondoa kwenye mazungumzo Jumatano wiki hii bila kufikia makubaliano na kimetishia kufanya migomo ya kitaifa kwa muda usiojulikana kuanzia tarehe saba mwezi ujao wa Januari.

Chama cha GDL kinataka nyongeza ya mshahara kati ya asilimia 10 na 30. Madereva wa treni wa Ujerumani ni miongoni mwa wafanyakazi wanaolipwa mishara mibaya zaidi barani Ulaya.