1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbappe kuihama PSG?

20 Mei 2019

Kylian Mbappe amejinyakulia tuzo mbili za mchezaji binafsi baada ya msimu wa kuridhisha na timu yake ya Paris Saint Germain.

https://p.dw.com/p/3ImF0
Paris Ballon d'Or Verleihung Mbappe Kopa Trophy
Picha: Reuters/B. Tessier

Mbappe alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na mchezaji bora mwenye umri mdogo.

Lakini ameonyesha mashaka iwapo ataendelea kuwa mchezaji wa PSG msimu ujao licha ya kuthibitisha mwezi Machi kwamba hataihama klabu hiyo ya Ufaransa.

Mbappe amesema amefikia sehemu katika taaluma yake ya soka sasa ambapo anaanza kupata ufanisi na anatarajia kuendelea hivyo iwe ni hapo PSG au katika klabu nyengine Ulaya.