1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchele uliooza umerejeshwa nchini China kutoka DRC

18 Septemba 2009

Shehena ya kwanza ya tani mia sita ya mchele unaoripotiwa kuoza imerejeshwa nchini China kutoka DRC.

https://p.dw.com/p/JkDt

Hatua hiyo ilichukuliwa na serikali ya Kongo kufuatia uchunguzi wake kwamba mchele takriban tani elfu sita ulioagizwa na kampuni ya kibinafsi ya CONGO- FUTUR ulikuwa umeoza.

Hatua hiyo inapokelewa vyema na wakaazi wa kinshasa na wale wa Bas-Congo ambao walitarajiwa kutumia chakula hicho.

Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo amefuatilia kisa hicho na ametutumia taarifa ifuatayo kutoka MATADI( jimboni Bas-Congo kusini magharibi mwa DRC)

Mwandishi: Salehe Mwanamilongo

Mhariri: Mohamed Abdulrahman