1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Medali ya dhahabu ya Usain Bolt-safi ?

17 Agosti 2009

Hakuna mashindano leo bila kutiliiwa shaka za doping au ?

https://p.dw.com/p/JD2f
Usain BoltPicha: AP

Baada ya ushindi wake wa kusismua ajabu wa mbio za mita 100 na rekod ya dunia ya sek.9.58,Usain Bolt wa Jamaica, anarudi leo uwanjani mjin Berln kulenga medali nyengne ya dhahabu na pengine rekod mpya katka mbio za masafa ya mita 200.

Katka masafa haya, ni yeye mwenye rekodi ya dunia ya sek.19.30. Bolt ameshasema hatazamii rekodi nyengine katika mita 200,lakini, atatimka mbo kama awezavyo. Je, tutazamie basi rekodi nyengine mpya ya dunia ?

Hakuna mbio katika orodha ya mashindano ya riadha -Athletics-zilizopata sifa mbaya kwa madhambi ya doping kama mita 100. Labda ,kisa kiilichohanikiza mno, ni kile cha Mkanada wa asili ya Jamaica BEN JOHNSON aliiegunduliwa na madhambii hayo wakati wa mashindano ya Olimpk ya Seoul,Korea ya Kusini 1988 na kutimuliwa nje ya kijiji cha olmpk baada ya kuvulwa taji la mta 100.

Kwa muda aliochukua juzi usiku Usain Bolt wa sek.9.58 -muda wa kusangaza ajabu uliofuta rekodi yake binafsi ya mwaka jana katika michezo ya olmpk ya Beijing wa sek.9.69 na baada ya medali zake 3 za dhahabu za olimpik ,analenga sasa kutwaa medali nyengne 3 za ubingwa wa dunia.Hii inawafanya watu kujiuliza: ilkuaje mjamaica huyu anaweka rekod za dunia moja baada ya moja kama mchezo ?

Uchambuzi wa Volker Hirth :

Bila shaka harufu ya madhambi ya doping humuandama kila mrushaji mkuki-(Javelin),kisahani cha chuma (discus) anaporusha.Mtu awe mpumbavu au mwenye kuamn sana kusadiki kweli,yanafanyika mashindano safi kabisa .

Ubaya wa mambo ni kwamba hakuna alama maalumu za kumta mbulisha kila mrushaji mkuki au kiksahani cha chuma anaetumiwa mada ya kutunisha msuli.Misuli ilitutumka mapajan na mabegani hujipatia mwanaradha yeyote katika mazowezi makubwa hata pia kwa kula musl na matunda.Enz za kutunisha misuli kwa madawa ya "Anabolc Steroide " zimepita hata zile za kumgundua mfanya madhambi hayo kwa alama za vipele usonii mwake.

Madhambi ya dopng hiii leo nii dhaifu sana kwa kuwa hayagunduliki na mbaya zadi hayawezi kuthibtshwa kwa aliefanya.Naamini, vitu vya kuongeza uhodari hivi sasa viimeinga awamu ya kiufund -ufundi ambao wataalamu wa kisayansii hawaumudu tena.Kwani, kumeza vidonge kumepita zamani.Na hapo, ndipo daraja ya kisasa ya uchunguzi ya wapigavita madhambi hayo walipofikia.Hivi sasa hutumwa (hormons) za kukua mwanada mu ambazo taabu kuziingundiia mwilini au nsulin kutoka mwilni mwa binadamu mwenyewe.Na kwavle hii pia inafahamika hivi sasa, tayarii imeshapitwa na wakatii.

Labda ,wafanyao madhambi ya doping, tayari wameshagundua matumizi ya viini vya mwanadamu-Gen-Doping.Huu ni utaratibu pekee wa kisayansi ambao unaweza tu kutumika kwa riidhaa na msaada tu wa Taasisi ya kiseriikali.Labda, mfumo huo upo kiswani Jamaica ,ambako ghafula nyota wote wa mbio za kasi hi leo wanatoka na hakuna awezae kutoa kielzo ilikuaje kawa hivyo ?

Nadhani, hakuna mwenye mapenzi makubwa ya michezo, atakadharau haya yote yanayopita au kuyafumbiia macho na kuridhia mashiindano makuu ni ya mashetani wakubwa na juu ya hivyo, wanavutia jinsi wanavyotamba.Mfano, kuuona mbio za kasi kabisa alizoonesha mwanadamu bila kujali alitumia chombo gani kujipatia kasi hyo.

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mharir:Othman Mirajii