1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya Misaada ya Libya,yatia nanga Misri

15 Julai 2010

Israel yaizuwia kufunga gati katika ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/OLk4
Waziri wa Mambo ya kigeni wa Misri, Ahmed Aboul Gheit,athibitisha meli ya misaada ya Libya imetia nanga Misri.Picha: picture-alliance/ dpa

Meli iliyobeba shehena ya misaada ya kiutu kwa ajili ya wapalestina inayotokea Libya,tayari imetia nanga katika bandari ya El-Arish ya Misri, ikisubiri maelekezo kutoka kwa maafisa wa serikali ya nchi hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa meli hiyo imebeba misaada ya madawa na vyakula ,inasubiri maelekezo hayo,ili kuweza kuruhusiwa kutumia mpaka wa Rafah,kilometa 40 kutoka bandari hiyo.

Mkurugenzi wa bandari ya el - Arish Jamal Abdelmaksoud ameeleza kuwa anasubiri maelekezo kutoka kwa viongozi wa serikali,ambapo atakuwa na mkutano na gavana wa Sinai ya Kaskazini,Murad Mowafi ili kuamua utaratibu wa kutumika kuiruhusu meli hiyo ijulikanayo kama ``Amalthea``,kufikisha misaada hiyo kwa wakaazi wa Gaza.

Meli hiyo hapo awali ilikuwa ikielekea moja kwa moja ukanda wa Gaza,kabla ya Israel kuizuia kufunga gati katika eneo hilo,ambapo Kapteni wa meli hiyo,alikubali masharti yaliyotolewa na Israel,na kuamua kurejea bandari ya el-Arish ya Cairo,na kusubiri utaratibu mpya kutoka Misri.

Meli mbili za Israel,ziliizingira meli hiyo ambapo kapteni wa meli hiyo,alieleza kuwa ilikumbwa na tatizo katika injini yake,jambo lililoilazimu kwenda kwa mwendo wa polepole mno.

Jumla ya wanaharakati 15 wa kipalestina,lakini wengi wao ni raia wa Libya,raia wa Nigeria,Algeria na Morocco,Haiti,Syria na India wanatajwa kuwa ndani ya msafara huo.

Misaada ikiwa na tani 2,000 ya misaada ya kiutu imeelezwa kuwa imetolewa na taasisi ya kimataifa ya misaada ya Gaddafi,ilitumia mawasiliani ya redio na bandari ya Misri,ili kuomba ruhusa ya kufunga gati nchini humo,kufuatia kuzuiwa na meli za kijeshi za Israel,kuingia ukanda wa Gaza.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Misri Ahmed Aboul Gheit amewaambia waandishi wa habari kuwa, serikali ya nchi hiyo imeiruhusu meli hiyo kufunga gati katika bandari hiyo,na kueleza kuwa mizigo iliyo ndani ya meli hiyo,itapakuliwa na kukabidhiwa kwa ilani nyekundu,ili kuifikisha kwa wakaazi wa Gaza.

Hali hiyo,imeondoa uwezekano wa kuzuka upya kwa mashambulio ya kijeshi ya Israel dhidi ya meli hiyo,ambapo tukio la uvamizi wa meli kama hizo za misaada mei,31 mwaka huu,na kusababisha vifo vya wanaharakati 9, lilisababisha taifa hilo kujikuta katika mbinyo mkubwa kutoka jumuiya za kimataifa.

Baada ya tukio hilo,Israel licha ya kukubali kufanyika kwa uchunguzi wa ndani,na kukataa kufanyika uchunguzi huru,ilikubali kupunguza vizuizi katika ukanda huo,na kueleza kuwa watazuia silaha na bidhaa zingine ambazo zitaweza kutumika kama silaha na kundi la kiislamu la Hamas,linalotawala eneo la Wapalestina.

Uchunguzi wa ndani uliofanywa na Israel,na kutolewa mapema wiki hii umeeleza kuwa uvamizi uliofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo Mei 31,na kusababisha vifo vya wanaharakati 9,kuwa licha ya kuwepo kwa makosa yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo,lakini matumizi ya nguvu yaliyofanywa ni ya haki,matokeo ambayo yalikuwa yakitarajiwa na wengi.

Wakati huo huo,Chama cha kuwasaidia watu masikini na walioteswa cha Libya,kimeruhusiwa kutumia dola milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa makazi yaliyoharibiwa huko Gaza,na kuzifanyia ukarabati mpya nyumba 500 zilizobomolewa kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara katika ukanda huo.

Mwandishi; Ramadhan Tuwa/ DPA

Mhariri;Abdul-Rahman