1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel adai adhabu kali

5 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Ckeo

BERLIN:

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani ameitisha hatua kali zaidi wachukuliwe vijana wanaofanya uhaliu wa matumizi ya nguvu.Kanzela Merkel, akasema kwamba mahkama zipewe uwezo wa kutoa adhabu za kuwatia korokoroni chipukizi hao .

Waziri mkuu wa jimbo la Hesse,Roland koch anaekabili uchguzi mwishoni mwa mwezi huu, ameigeuza mada hii jukwaa la usoni la kampeni zake.Ni sehemu ya mpango wake wa mambo 6 ya kuzima uhalifu unaofanywa na chipukizi.