1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yabadilisha sera yake ya uhamiaji

Ambia Hirsi14 Novemba 2015

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametetea uamuzi wa Ujerumani kubadilisha sera yake juu ya wakimbizi na kusisitiza msimamo wa taifa hilo juu ya suala la uhamiaji.

https://p.dw.com/p/1H5r6
Angela Merkel zu den Terroranschlägen in Frankreich
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Kansela wa Ujerumani angela Merkel imetetea uamuzi wa ujerumani kubadilisha sera yake juu ya wakimbizi na kusisitiza msimamo wake kuhusu suala la uhamiaji na kusema kwamba ataendeleza juhudi za kuwapa hifadhi wakimbizi.

Muongozo wa sheria ya Dublin juu ya wakimbizi inasema watu wanaotafuta hifadhi barani ulaya wanastahili kutoa maombi ya kupewa hifadhi katika taifa la kwanza wanaloingia barani ulaya. Merkel alifitilia mbali sheria hiyo mwezo agosti mwaka huu kwa wakimbizi wa syria wanatoroka ghasia nchini mwao. Majuma matatu yaliyopita waziri wa masuala ya ndani wa ujerumani Thomas de Maiziere aliimarisha usalama mpakani lakini Merkel ametetea uamuzi huo katika mahojiano ya moja kwa moja katika runinga bila kufafanua mpango maalum juu ya hatma ya wakimbizi nchini Ujerumani

Pressekonferenz Thomas de Maiziere
Waziri wa mambo ya ndani Thomas de MaizierePicha: Getty Images/AFP/T. Schwarz

Merkel amekuwa akikabiliwa na wakati mgumu kutoka kwa wapinzani wake juu ya suala la wakimbizi anapojiandaa kukutana na viongozi wengine duniani ambao pia wanajitahidi kupunguza miminiko mkubwa wa wakimbizi hao barani ulaya.

Tunaweza kumudu wahamiaji

Kwa kutumia maneno "bila shaka tutamudu" ambayo yanaonekana kuwashawishi wanaopinga sera yake juu ya uhamiaji " Merkel anamatumaini ataweza kubadili mioyo ya wapinzani wake lakini hoja hiyo imepata mafanikio madogo kuwavuta washirika wa Ujerumani katika muungano wa Ulaya kusaidiana naye kubeba mzigo wa wakipizi. Kura za maoni zinaonyesha kuwa umaarufu wa Merkrl unaendelea kudorora.

Siku za hivi karibuni, uongozi katika muungano wake umekuwa ukitofautiana juu ya mpango wa kuondoa vikwazo kwa wahamiaji wasyria waliopewa hifadhi hali ambayo ingeweza kuwaruhusu kuwaleta jamaa zao Ujerumani kwa miaka miwili. Mpango huo uliotangazwa na Waziri wa mambo ya ndani bila ufahamu wa Merkel na kusitishwa baada ya pendekezo hili kuungwa mkono na wahafidhina maarufu. Hatua ambayo ilizua malumbano na cheche za maneno kutoka kwa viongozi mbali mbali nchini Ujerumani.

Changamoto ya Merkel

Japo nyakati ni ngumu kwa Kansela Angela Merkel haonekani kukatizwa tamaa na wapinzani wake na badala yake anaelenga kuimarisha sera ya uhamiaji kwa kuweka vizuizi zaidi bila kuathiri kwa mapana chanya yake. Merkel Pia anahitaji kupatanisha maslahi ya uongozi wa muungano wa kulia na kushoto.

Kwa miaka mingi, vitendo yake ndani na nje ya nchi yamempatia uwezo mkubwa wakutokabiliwa na upinzani kama kiongozi Ujerumani na hata miongoni mwa wanasiasa wengi kwa Ulaya,Lakini sifa hiyo huenda ikatiwa doa na msimamo wake juu ya suala la wakimbizi.