1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel awalaani maadui wa hadhi ya mwanadamu

Admin.WagnerD26 Agosti 2015

Kansela Angela Merkel amesema chuki dhidi ya wakimbizi haitavumiliwa. Ameyasema hayo baada kuwasili kwenye kituo cha wakimbizi mjini Heidenau kilichoshambuliwa wiki iliyopita .

https://p.dw.com/p/1GLkz
Kansela Angela Merkel awatembelea wakimbizi katika mji wa Heidenau
Kansela Angela Merkel awatembelea wakimbizi katika mji wa HeidenauPicha: Getty Images/AFP/T. Schwarz

Kansela Merkel amesema baada ya kuwasili kwenye mji huo wa Heidenau kwamba itikadi ya mrengo mkali dhidi ya wakimbizi haitavumiliwa. Kansela Merkel ameilaani vikali itikadi hiyo .Ametamka kuwa kuheshimiwa hadhi ya kila mtu ni jambo linaloeleweka na kila mtu nchini Ujerumani

Mwishoni mwa wiki iliyopita polisi walipambana na watu wenye itikadi kali za mrengo wa kulia walioafanya fujo kwenye kituo hicho cha wakimbizi kilichopo mashariki mwa Ujerumani.

Sehemu kadhaa zinazotumiwa kwa ajili ya kuwaweka watu wanoomba hifadhi ya ukimbizi nchini Ujerumani zimeshambuliwa na makundi ya watu wenye itikadi kali.

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck leo pia ameitembelea nyumba moja ya kuwahifadhia wakimbizi, katika kitongoji cha Berlin-Wilmersdorf mjini Berlin .Rais Gauck aliwapongeza wanafunzi,madaktari na wananchi wengine waliojitolea kuwasidia wakimbizi.

Rais wa Ujerumani amewapongeza watu hao kwa kuionyesha nuru ya matumaini nchini Ujerumani kinyume na habari juu ya mashambulio yanayofanywa katika nyumba za kuwahifadhia wakimbizi.

Rais wa shirikisho la Ujerumani Jaochim Gauck akiwatembelea wakimbizi katika moja ya vituo vya kuwahifadhi mjini Berlin. Gauck amesema Ujerumani itaimudu changamoto ya ongezeko la wakimbizi na kulaani makundi ya chuki dhidi yao.
Rais wa shirikisho la Ujerumani Jaochim Gauck akiwatembelea wakimbizi katika moja ya vituo vya kuwahifadhi mjini Berlin. Gauck amesema Ujerumani itaimudu changamoto ya ongezeko la wakimbizi na kulaani makundi ya chuki dhidi yao.Picha: Reuters/S. Loos

Watu karibu 800,000 wanatarajiwa kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini Ujerumani mnamo mwaka huu . Hata hivyo Kansela Merkel amesema haitawezekana kwa Ujerumani kutoa hifadhi kwa kila mwananchi wa Umoja wa Ulaya ambae hana ajira katika nchi yake.

Kansela amekutana na wakimbizi,wafanyakazi wanaowasaidia wakimbizi na wakaazi wa mji huo wa Heidenau. Polisi kadhaa walijeruhiwa kutokana na kushambuliwa kwa kurushiwa chupa na vijana wanaowachukia wakimbizi.

Ujerumani inakabiliwa na wimbi kubwa la wakimbizi na maafisa wametabiri kwamba idadi ya w akimbizi hao inaweza kuvuka,800,000 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Wakati idadi kubwa ya Wajerumani wapo tayari kuwakaribisha wakimbizi hao, wapo wachache miongoni mwao wanaowapinga wakimbizi hao.

Katika kipindi kilichopita cha nusu mwaka mashambulio zaidi ya 200 yalifanywa dhidi ya wakimbizi nchini Ujerumani.

Mwandishi:Mtullya Abdu./ape,dpa,

Mhariri: Yusuf Saumu