1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel katika Baraza la Ulaya

16 Aprili 2008

Kanzela wa Ujerumani Angela Merkel ahutubia Baraza la Ulaya huku haki za binadamu zikiwa mada yake kuu.

https://p.dw.com/p/Dit1
Kanzela Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, kabla kulihutubia Baraza la Ulaya mjini Strassbourg alisema "Maswali ya kiuchumi na yale ya haki za binadamu si lazima yapingane."

Jukwaa barabara la kuzungumzia hayo ni Baraza la ulaya mjini Strassbourg,Ufaransa.

Kanzela Merkel pia ametaja jukumu la kuingilia kati ndani ya mambo ya nchi nyengine ikilazimika.

Kanzela wa zamani wa ujerumani,Konrad Adenauer mara moja aliliita Baraza la Ulaya "hisia za Ulaya".Tangu 1949 lipo Baraza hili na leo lina wanachama 47 -hivyo ni kusema nchi zote za Ulaya ni wanachama.Baraza hili lisichanganywe na Tume ya Umoja wa Ulaya-European Commission mjini Brussels.

Baraza la Ulaya tangu kuasisiwa kwake limekuwa likipigania , kutetea na kuyaeneza maadili na desturi za Ulaya -mfano wa demokrasia,kufuata sheria na mbele kabisa kuheshimu haki za binadamu.

Pale Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani atakapolihutubia Baraza hilo la Ulaya ,mada yake itakua moja tu-haki za binadamu.

Kanzela angependa kutupa jicho lake katika kazi inayofanywa na Mahkama ya Ulya iliopo huko na kwa kuwa katika swala la haki za binadamu kuna mengi ya kufanya hata barani Ulaya ,ziara yake katika Mahkama hiyo imebainisha wazi.

Raia yeyote wa ulaya anaehisi haki yake imekanyagwa, ana haki ya kupeleka kesi yake mbele ya Mahkama hiyo.

Kiasi cha kesi 40,000 zilifika kwenye Mahkama hiyo ya ulaya mwaka uliopita tu .

Mageuzi ya Mahkama hii na jinsi inavyofanya kazi yakihitajika kitambo sasa.Lakini katika wakati wa Wladmir Putin akiwa rais wa Urusi, akipinga vikali kuidhinisha azimio la kufanya mageuzi hayo.

Ndio maana kanzela Merkel amewalenga wajumbe wa Urusi moja kwa moja katika hotuba yake mbele ya wajumbe wa Baraza hilo la Ulaya :

"Natumai wakati umewadia kwa Bunge jipya la Urusi (Duma) kuyatupia jicho jipya mapatano 14 zaidi na kuyaidhinisha.

ikifanyika hivyo nitafurahi sana."

Kanzela Merkel hakuuzungumzia moja kwa moja mgogoro wa China na Tibet, lakini katika matamshi yake mengi alitoa ishara anamkusudia nani katika ila alizotoa.

Matumizi ya nguvu na mkomoto yasiwe ufunguo wa kutatua matatizo ya jamii za wachache nchini-alisema.

Na alipozungumzia maadaili na desturi za pamoja za Ulaya nio msingi,Kanzela Merkel alitaja haki za binadamu haziwi swali la ndani la nchi yoyote,na hii ilibainisha dhahiri akizikusudia nchi kama Urusi na China.

"Ni uzuri kuona barani ulaya, kuna jukumu la kila mmoja kuweza kuingilia yanayotendeka kwa mwenziwe.Katika swali la haki za binadamu, hakuna mwiko kutoingilia yanayopita ndani ya mwenzio ili kujikinga na tuhuma- kwa mfano za makamishna wa haki za binadamu."

Alisema Kanzela Angela Merkel.

Hata nchi za Ulaya -alisema Kanzela Merkel, zinapaswa kujiuliza tena na tena na kujikosoa katika kulinda ya haki za binadamu.kila mmoja anahukumiwa kwa vitendo vyake.