1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MESEBERG : Merkel na Chirac wajadili Airbus

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPA

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Jaques Chirac wa Ufaransa wametowa wito wa kugawana kwa msingi wa haki mzigo wa kuiunda upya kampuni ya Airbus ya kutengeneza ndege barani Ulaya.

Viongozi hao wametowa taarifa ya wito wao huo kufuatia mazungumzo yao mjini Meseberg kaskazini mwa mji mkuu wa Ujerumani Berlin.Chirac baaade aliwaambia waandishi wa habari yeye na Merkel wana imani kwamba uongozi wa kampuni ya Airbus utachukuwa maamuzi ya haki wakati utakapoamuwa juu ya upunguzaji wa ajira na ufungaji wa viwanda vyake katika nchi zote mbili za Ufaransa na Ujerumani.

Kampuni ya Airbus inaajiri takriban watu 21,000 katika sehemu zake saba nchini Ujerumani na maafisa wa Ujerumani wana wasi wasi kwamba sehemu hizo ndio zitakazoathirika na upunguzaji huo wa wafanyakazi.