1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi apanga kukutana na kijana mdogo wa Afghanistan

2 Februari 2016

Mchezaji nyota wa Barcelona Lionel Messi ana matumaini ya kupanga kukutana na kijana mdogo wa Afghanistan ambaye amejipatia umaarufu kwenye mitandao ya intaneti

https://p.dw.com/p/1HnQe
Mortaza Ahmadi Lionel Messi Fan Afghanistan
Picha: Mahdi Ahmadi

Picha ya mtoto huyo wa Kiafghanistan akiwa amevalia jezi ya plastiki yenye rangi ya jezi ya timu ya taifa ya Argentina kusambaa kote duniani, limesema shirikisho la kandanda nchini Afghanistan leo.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka mitano Murtaza Ahmadi ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo nyota kutoka Argentina lakini kupata jezi ya mchezaji huyo nyota anayemshabikia si rahisi kwa familia yake masikini kutoka jimbo lenye matatizo ya vita la Ghazni karibu na mji mkuu Kabul.

Jorge Messi , baba wa Lionel , ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumamosi kwamba mchezaji huyo nyota ameiona picha hiyo katika mitandao ya kijamii na anataka kufanya kitu kwa shabiki wake huyo.

Wakati huo huo mshambuliaji nyota wa Barcelona Neymar pamoja na rais wa zamani wa klabu hiyo walifikishwa kizimbani leo mjini Madrid ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusiana na ukiuakji wa sheria za uhamisho wa wachezaji kuhusiana na mchezaji huyo kutoka Brazil.

rais wa klabu hiyo Josep Bartomeu na mtangulizi wake Sandro Rosell waliwasili pamoja kujibu maswali ya jaji Jose de la Mata kuhusiana na uhamisho wa Neymar kutoka klabu ya Santos ya Brazil kwenda barcelona.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga