1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi, Ronaldo na Ribery nani bora?

16 Desemba 2013

Lionel Messi, Franck Ribery na Cristiano Ronaldo wameorodheshwa kuwania tuzo ya mwaka huu ya Ballon d'Or. Kwa mujibu wa Shirikisho la FIFA na Jarida la Kandanda la Ufaransa ambalo ni mfadhili

https://p.dw.com/p/1AVXg
Finalisten bei der Wahl zum Weltfußballer des Jahres: Franck Ribéry, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo
Picha: Getty Images

Mshambuliaji wa Barcelona Messi ameshinda tuzo hiyo mara nne lakini lakini anaonekana kulikosa mwaka huu, baada ya msimu wake kuathirika kutokana na jeraha. Mchezaji wa Ufaransa Franck Ribery alikuwa sehemu ya timu ya Bayern Munich iliyotwaa mataji matatu mfululizo ya Champions League, Bundesliga na Kombe la Shirikisho la Ujerumani pamoja na Kombe la European Super Cup.

Mshambuliaji nyota wa Ureno anayechezea Real Madrid Christiano Ronaldo maarufu kama CR7 alishinda Ballon d'Or mwaka wa 2008 na amepigiwa upatu kulishinda tena mara hii. Mshindi atatajwa mjini Zurich Januari 13.

Jupp Heynckes aliyekuwa kocha wa Bayern Munich atawania taji hilo kwa upande wa kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, pamoja na kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson na Jurgen Klopp wa Borussia Dortmund.

Kwa wanawake, Ralf Kellermann (VfL Wolfsburg), Silvia Neid (timu ya taifa ya Ujerumani) na Pia Sundhage (timu ya taifa ya Sweden) ndio walioteuliwa. Nadine Angerer (Ujerumani), Marta (Brazil) na Abby Wambach (Marekani) ndio wagombea watatu wanaowania tuzo ya Mchezaji bora mwanamke.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman