1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO CITY : Steinmeir ziarani Mexico

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9D

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir yuko nchini Mexico katika kituo cha kwanza cha ziara ya siku tano ya Amerika Kusini.

Steinmeir amekuwa na mazungumzo na waziri mwenzake wa Mexico Patricia Espinosa na anatazamiwa kukutana na Rais Felipe Calderon wa Mexico.Waziri huyo wa Ujerumani atafunguwa jengo la ubalozi wa Ujerumani mjini Mexico City na pia anatarajiwa kutia saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Ujerumani ni mshirika wa nne mkubwa wa kibiashara kwa Mexico.

Ziara ya Steinmeir pia itamfikisha Panama na Jamhuri ya Dominica.