1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfumo wa SMS watumika kuwasajili watoto

8 Desemba 2015

Watoto wengi hawasajiliwi baada ya kuzaliwa na hawapati vyeti vya kuzaliwa. Mtaalamu kijana wa kompyuta nchini Ivory Coast amepata suluhu ya tatizo hili kubwa.

https://p.dw.com/p/1HJK0
DW Sendung Africa on the Move - Elfenbeinküste Geburtenregistrierung
Picha: DW

Mfumo wa SMS watumika kuwasajili watoto

Asilimia 60 pekee ya watoto duniani wanasajiliwa, bila vyeti vya kuzaliwa hawawezi kwenda shule kufuatia kukosa kuwa na cheti hicho, sasa mtaalamu wa masuala ya Kompyuta amepata suluhu ya tatizo hilo kubwa.

Elimu nzuri ya shule, labda chuo kikuu baadaye kisha upate kazi nzuri. Wazazi wanachohitaji ni maisha mazuri kwa watoto wao. Lakini hili halifanikiwi katika mataifa mengi ya kiafrika kwa sababubau ya kukosa utaratibu unaopaswa kuwepo. Watoto wengi hawasajiliwi baada ya kuzaliwa na hawapati vyeti vya kuzaliwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia watoto UNICEF linakadiria idadi ya watoto ambao hawajasajiliwa kufikia milioni 3 nchini Ivory Coast pekee. Shirika hilo linaendelea kukadiria kwamba asilimia 60 ya watoto wachanga duniani wanasajiliwa. Mtaalamu kijana wa masuala ya Kompyuta sasa amepata jibu ya tatizo hilo.