1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa kiisiasa wazidi makali Venezuela

Oumilkheir Hamidou
30 Aprili 2019

Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Juan Guaido akiwa pamoja na mwanaharakati Leopoldo Lopez na kundi dogo la wanajeshi waliokuwa na silaha amewatolea wito wanajeshi wampindue rais wa kisoshalisti Nicolas Maduro.

https://p.dw.com/p/3HiTy
Venezuela Juan Guaido
Picha: Reuters/C. G. Rawlins

"Nnataka kuwaambia wananchi wa Venezuela; Wakati ndio huu umewadia wa kuteremka majiani na kufuatana na wanajeshii hawa mashujaa"amesema hayo Leopoldo Lopez aliyekuwa akishikiliwa jela tangu mwaka 2014 kwa kuongoza maandamano dhidi ya serikali."Kila mtu anabidi ateremke majiani kwa amani" amesisitiza. Lopez amesema ametolewa katika kifungo cha nyumbani na vikosi vya usalama vilivyoitika amri ya Guaido anaetambuliwa na Marekani na dazeni kadhaa ya serikali nyengine kama kiongozi halali wa Venezuela.

Na huku akihutubia kutoka barabara kuu, vikosi vitiifu kwa rais maduro vimefyetua  gesi za kutoa machozi kutoka ndani ya kituo cha jeshi la wanaanga huku maamia ya watu waliokuwa wakipeperusha bendera ya Venezuela wakiwashangilia.

Wakati ndio huu "amesema mwanajeshi mmoja kijana aliyefunika uso wake.Tukio hilo lililojiri katika eneo wanakoishi matajiri mashariki mwa mji mkuu Caracas halikuwazinduwa wananchi walio wengi.

Wanajeshi wa Venezuela katika kituo cha jeshi la wanaanga cha Miranda
Wanajeshi wa Venezuela katika kituo cha jeshi la wanaanga cha MirandaPicha: Reuters/C.G. Rawlins

Wito wa Guaido haukuitikwa na waanchi walio wengi wa Caracas

Waziri wa ulinzi Vladimir Padrino amezungumzia kupitia mtandao wa twitter kile alichokiita "njama potofu ya kusababisha vurugu na vitisho. Wakati huo huo mkuu wa chama cha kisoshalisti Diosdado Cabello amesema wakaazi wengi wa Caracas wametulia na kuwatolea wito wafuasi wa serikali wakusanyike katika kasri la rais kumlinda Maduro kutoka kile alichokiita njama inayoungwa mkono na Marekani."Tunakwenda katika kasri la Miraflores kulinda mapinduzi, kumlinda Nicolas na kulinda utawala wa Hugo Chavez" amesema Cabello kwa njia ya simu kupitia televisheni ya taifa.

Baadae vikosi vya usalama vilivyopanda mapikipiki vilifyetua gesi za kutoa machozi kuwatawanya watu waliokusanyika katika daraja. Haijulikani lakini kama kuna waliojeruhiwa.

Sauti zimeanza kupazwa kati ya wanaolaani na wale wanaounga mkono tukio hilo. Katika wakati ambapo mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani John Bolton anawataka wanajeshi wa Venezuela walinde katiba na wananchi, rais wa Bolivia Evo Morales na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Cuba Bruno Rodrigues wanalaani njama ya mapinduzi.

Serikali ya mpito ya Uhispania imetoa wito wa kipindi cha mpito cha amani kuelekea uchaguzi wa kidemokrasi wa rais.Wito kama huo umetolewa pia na Umoja wa ulaya.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AP/

Mhariri: Daniel Gakuba