1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea Urais wa Republican amwagia sifa Putin

9 Agosti 2016

Mgombea urais wa Marekani wa chama cha Republican angemwagia sifa rais wa Urusi, anasifu sera ambazo jumuiya ya kujihami ya NATO inazipinga na kwamba anadokeza kukubaliana na hatua ya Urusi kulitwaa eneo la Crimea.

https://p.dw.com/p/1JeYE
USA Donald Trump
Picha: Reuters/C. Allegri

Vyombo vya habari vya Marekani vinazungumzia kwa muda sasa kile kilichopewa jina "bro-mance", kati ya wanaume hao wawili Donald Trump na Vladimir Putin. Bro-mance ikiwa na maana uhusiano kati ya ndugu, lakini tafsiri hiyo si sahihi kwani kuna mengi tofauti yanayoweza kuzungumziwa kuwahusu viongozi hao wawili. Haijabainika wazi dhihiri shahiri kama Trump na Putin wameshawahi kukutana.

"Sijawahi kukutana na Putin na simfahamu. Amesema jambo zuri kunihusu: Mimi ni mwerevu. Hilo tu. Sijawahi kukutana naye."

Lakini katika mahojiano ya awali Trump amewahi kusema kinyume kabisa na hayo. alisema Trump

"Ndiyo nina mawasiliano na Putin. Na ninaweza kukwambia Putin ni mtu mzuri sana, kile ambacho mimi na wewe tunakifanya hapa leo. Na ndivyo alivyo hata ukimuangalia kwa namna yoyote." aliongeza

Trump aliitoa kauli hiyo mwishoni mwa mwaka 2013, kiasi miaka miwili na nusu iliyopita. Mwishoni mwa wiki iliyopita kituo cha matangazo cha Marekani, ABC, kilimuweka Trump katika kiti moto kuhusiana na matamshi yake yanayokinzana.

Trump alisema haamini kwamba ameshawahi kukutana na Putin. Lakini alipoambiwa na mtangazaji aliyekuwa akimhoji kwamba yeye lazima awe anafahamu ni wakati gani alipokutana naye, Trump alijibu akiseka, "Ndiyo, nafikiri hivyo."

Je hizo ni dalili za tatizo la kusahausahau la mtu mwenye umri wa miaka 70? Au je Trump anataka kuficha kitu? Waandishi kadhaa wa habari wameshafanya utafiti: Hakuna mkutano wowote kati ya Trump na Putin uliowahi kufanyika na kurekodiwa. Wakati Trump alipoandaa mashindano ya urembo ya "Miss Universe" mjini Moscow miaka mitatu iliyopita, alitaka sana kwamba Putin awe mgeni wa heshima. Lakini Putin hakuhudhuria.

Russland Yevgeny Zinichev
Picha: picture alliance/dpa/TASS/A. Korotayev

Waandishi wengine wa habari wanadhani Trump ana uhusiano wa siri na wafanyabiashara matajiri wa Urusi na anapokea fedha kutoka Urusi; Tetesi ambazo zinaonekana kumgusa moja kwa moja Trump kwa sababu amekuwa akikataa kata kata kuwasilisha nyaraka kuonyesha jinsi alivyokuwa akilipa kodi. Aliwahi kuwa na mipango ya kujenga mnara wa Trump, Trump Tower na Hoteli ya Trump, Trump Hotel, mjini Moscow. Mipango hiyo lakini ilikufa. Pia jaribio la kutengeneza mvinyo wa Trump, Trump Vodka, halikufua dafu.

Pongezi za heshima lawa jambo la wasiwasi

Pongezi za kuheshimiana kati ya Trump na Putin ni suala la aina, anasema Michael O'Hanlon, mtaalamu wa sera za kigeni wa Taasisi ya kutoka maoni na ushauri ya Brookings.

"Ni jambo linalotia wasiwasi kwamba sifa na haiba ya Trump inaonekana ndani ya Putin. Sisi mataifa yenye nguvu tunaugawa ulimwengu. Na Putin ataachiwa uwanja wake wa ushawishi ilimradi anaacha kulibeza eneo letu la ushawishi."

Lakini mshikamano kati ya nafsi ya Trump na Putin unatosha kuelezea kwamba kauli za Trump mara kwa mara zinasikika kana kwamba Putin amempa maelekezo kwa njia ya simu.

Trump anasema kwa mfano kwamba jumuiya ya kujihami ya NATO imepitwa na wakati. Ikiwa mataifa ya eneo la Balkan yatalindwa na Marekani, itategemea kama yanalipa michango yao kikamilifu. Na kuitambua rasmi hatua ya Urusi kulitwaa eneo la Crimea, kama alivyofanya Trump mwishoni mwa wiki iliyopita, hakuweza kufikria vizuri kama rais:

Kwa kipindi kifupi katika miongo kadhaa Trump ameitikisa misingi ya imani ya chama cha Republican. Uzalendo badala ya ushirikiano wa kimataifa. Kulilinda soko la Marekani badala ya biashara huru. Marekani kwanza badala ya jumuiya ya kujihami ya NATO. Mgombea urais wa chama cha Republican aliyemtangua Trump, Mitt Romney, ameieleza Urusi kuwa mpinzani nambari moja wa Marekani katika siasa za ulimwengu. Si ajabu kwamba rais Putin atafurahia Trump akiwa ikulu ya Marekani.

Mwandishi: Ganslmeier, Martin / Washington (NDR)

Tafsiri: Josephat Charo

Mhariri: Mohammed Khelef