1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege jijini London wanukia

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cert

LONDON:

Wafanyakazi ,katika baadhi ya viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi nchini Uingereza,wamepiga kura kufanya migomo mitatu mwaka ujao.Wafanyakazi katika viwanja saba vya ndege nchini humo,vikiwemo viwanja vya Gatwick na Heathrow vya mjini London,wameamua kugoma baada ya shirika la BAA kutangaza kubadilsha mpango wao wa mafaao ya wafanyakazi.Chama cha wafanyakazi cha The United Union ,kimeitisha migomo ya saa 24 kila mmoja tarehe 7 na 14 mwezi ujao wa Januari na kufuatia mgomo mwingine wa saa 48 kuanzia Januari 17.Akizungumza katika mkutano na wandishi wa habari hii leo,Bernard Gold,katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha wafanyakazi katika viwanja hivyo,amesema kuwa wanapanga mgomo mwezi ujao ambao unaweza kuvuruga safari za ndege pamoja na shughuli katika viwanja hivyo.Kampuni ya BAA,inayomilikiwa na Ferrovial kutoka Uhispania, imesema inasikitishwa na hatua hiyo na itafanya kila juhudi kupunguza usumbufu kwa abiria.