1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mhindi achaguliwa kuiongoza Deutsche Bank

27 Julai 2011

Mgogoro wa fedha Marekani,kuchaguliwa mhindi kuongoza benki mashuhuri ya Ujerumani Deutsche Bank,na mauwaji ya Norway ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa Ujerumani hii leo.

https://p.dw.com/p/124ru
Bendera ya NorwayPicha: dapd

Tunaanzia lakini Norway ambako wanasheria wanajiuliza kama mtuhumiwa wa mauwaji ya Oslo na Utoya anatambua alichofanya au la.Gazeti la Hessisiche/Niedersächsische Allgemeine linaandika:

Hata kama Anders Behring Breivik atatajwa kuwa "hazimtoshi",yungali bado hatari kwa jamii na anabidi amalizie maisha yake korokoroni.Uchunguzi ukionyesha "ana akili zake",basi mwendesha mashtaka atabidi apendekeze adhabu ya juu kabisa.Kwasababu miaka 21 jela kama adhabu ya juu mtu anapouwa ni kidogo sana.Ndio maana unachunguzwa uwezekano wa kuandamwa kuhusiana na uhalifu dhidi ya ubinaadam na kutolewa adhabu ya juu kupita kiasi.Na hapo linawajibika taifa linalofuata sheria la Norway.Taifa hili hili ambalo Breivik anapambana nalo,ndilo linalolazimika kudhihirisha lina nguvu zaidi kumshinda mhalifu.Hilo linawezekana kupitia kesi isiyokuwa na ila yoyote kisheria.Ni wajib wa Norway kwa wahanga wa nchi hiyo inayothamini uhuru na uvumlivu.

Barack Obama Pressekonferenz Budgetverhandlungen USA Juli 2011
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: dapd

Wanacheza na moto wanaotaka kuitumbukiza Marekani katika balaa la kushindwa kulipa madeni yake,linaandika gazeti la "Der neue Tag"

Hata kama watafanikiwa kwa wakati uliopangwa kufikia maridhiano ya kuongeza kiwango cha nakisi ya bajeti,lakini imani katika masoko ya hisa na ulimwenguni itaathirika.Yeyote yule mfano wa marepublican katika baraza la Congress anayeamini hakutakua na madhara yoyote kama Marekani itashindwa kwa muda mfupi kulipa madeni yake,anachangia kueneza hofu pengine rais mpya wa Marekani atakuwa wa kutoka chama cha Republican.

Deutsche Bank Symbolbild
Makao makuu ya Deutsche Bank mjini FrankfurtPicha: picture alliance/dpa

Mada yetu ya mwisho magazetini mchana huu inahusu kuchaguliwa mhindi kuongoza benki kubwa na mashuhuri kabisa ya Ujerumani Deutsche Bank.Gazeti la Badische Neueste Nachrichten linaandika:

Hasara ingekuwa kama Ackermann angeipa kisogo moja kwa moja benki hiyo.Kinyume kabisa,kuanzia mwaka 2012 anakwenda kuongoza baraza la usimamizi la benki hiyo.Ufumbuzi huo una walakini kwasababu huko Ackerman anaweza kuchunguza vizuri kama waliokabidhiwa wadhifa wake wanafuata nyayo zake..Kwa hivyo hakuna mabadiliko yoyote.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed