1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magaidi bado hawajakamatwa.

Schmidt Andrea7 Agosti 2008

Miaka 10 tokea Tanzania na Kenya zishambuliwe na magaidi.

https://p.dw.com/p/EreT
Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi baada ya kushambuliwa na magaidi.Picha: AP



Miaka 10 iliyopita magaidi walifanya mashambulio makubwa yasiyokuwa na mithili katika historia ya nchi za afrika mashariki.Katika mashambulio hayo kwenye balozi za Marekani mijini Nairobi na Dar Es Salaam watu zaidi ya mia mbili waliangamia.

Watu wengine wapatao alfu 5 walijeruhiwa.Waliotenda unyama huo bado hawajakamatwa hadi leo.

Serikali za Kenya ,Tanzania na Marekani zilishtukizwa na mashambulio hayo. Hatari ya mashambulio ya kigaidi nchini Kenya na Tanzania haiukutathminiwa kuwa kubwa , ingawa Kenya ina mpaka mrefu na Somalia ambao ulikuwa wazi, na ingawa mkuu wa magaidi Osama bin Laden bado alikuwa anaendesha shughuli zake kutokea Sudan hadi mwaka 1996.

Kizuizini Guantanamo

Mmoja wa watuhumiwa wa maandalizi ya mashambilio hayo Fazul Abdullah Mohammed raia wa Comoro aliponyoka kutiwa mbaroni mapema wiki hii. Mwengine Ahmed Khalfan Ghailani mwanachama wa Al Qaeda- na raia wa Tanzania amewekwa katika mahabusu ya Guantanamo inayosimamiwa na Marekani. Anatuhumiwa kuwa alifanya mashambulio hayo.Alikamatwa nchini Pakistan mnamo mwaka 2004 na kukabidhiwa kwa idara za Marekani miezi mitano baadaye.

Katika kukumbuka mwaka wa kumi tokea mashambulio hayo yafanyike nchini Kenya na Tanzania, wataalamu wanatahadharisha juu ya uwezekano wa Afrika Mashariki kushambuliwa tena.Sikiliza mahojiano na mhanga wa shambulio hilo aliyekuwa mfanyikazi kwenye ubalozi wa Marekani wakati huo.