1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 20 ya mkataba wa umoja wa mataifa wa kuzuwia mateso

Sekione Kitojo26 Juni 2007

Tangu miaka 20 iliyopita , tarehe 26 Juni 1987, mkataba wa umoja wa mataifa wa kupinga utesaji uliidhinishwa nchini Denmark, na ukapata uungwaji mkono muhimu na kuupa nguvu. Hata hivyo miaka mitatu ilipita kabla ya kuungwa mkono kikamilifu kwa kuweza kupata kuidhinishwa, haki za binadamu taratibu zilipata umuhimu katika siasa za kimataifa. Uendeaji kinyume haki za binadamu hata hivyo hadi sasa unaendelea, kama anavyoelezea Helle Jeppesen katika uhariri wake.

https://p.dw.com/p/CB3J
Picha: dpa

Mtu anayetumia nguvu, hasikilizi hoja zozote, inasema methali moja ya Kichina. Utesaji ni matumizi ya nguvu ya aina mbaya kabisa. Wahanga hawawezi kujitetea, wako wachache, haki zao zote zinaporwa, licha ya kuwa mkataba huu wa haki za binadamu unawahusu wao.

Hata hii leo baada ya miaka 20 ya kuidhinishwa kwa mkataba wa kupinga mateso, watu karibu kila mahali duniani wanateswa. Katika nchi ambapo mkataba huu unafahamika kwa miongo kadha , na katika mataifa ambayo kwa miongo kadha yanatajika kuwa yanademokrasia.

Majadiliano kuhusu utesaji kuanzia wakati wa tukio la shambulio la kigaidi la Septemba 11, yameonyesha wazi kabisa , ni vipi haki za binadamu zinavyoendewa kinyume, kinyume na sheria yenyewe inavyoeleza kuwa watu wasifanyiwe mateso.

Kinachoshangaza ni kuwa hata katika mataifa ambayo yanataka kusambaza haki hizi za binadamu duniani kote, wanajadili , iwapo inawezekana kufanya mateso kidogo, ili kuweza kuzuwia ugaidi wa kimataifa.

Hapa majadiliano yanakwenda kinyume na lengo. Mateso sio mbinu bora za kupata taarifa, bali kote duniani ni chombo kinacholeta ugaidi , na jamii ama kundi la jamii haliwezi kunyamazishwa na mbinu hii, ama kuudhoofisha upinzani, ili wenyewe mbaki madarakani.

Mbinyo na mateso mbinu hizi hazifai tena, na mbinu ya mateso kuweza kupata taarifa haileti tija yoyote.

Iwapo kucha zitang’olewa, ama kichwa kuingizwa majini mara kwa mara , mtu anaweza kabisa kukiri kila kitu kutokana na kuwa katika maumivu makali. Watu wengi katika hali hii watatoa taarifa tu za shambulio lililofanywa katika kituo cha biashara cha dunia world Trade Center, hata kama ilikuwa tofauti kabisa.

Kwa hiyo kutenda , kama vile ni mateso kidogo tu mara nyingine kwa dharura , kunaleta hali isiyofaa katika yale yaliyokubalika katika muda wa miaka 20 iliyopita.

Mkataba wa umoja wa mataifa wa kutotumia mbinu za mateso umeweza kufikia mafanikio fulani. Mojawapo ni kujisikia aibu kwa wale wanaoendeleza hukumu ya kifo. Leo hii hakuna taifa ama hata dikteta ambaye anapendelea kuweka wazi , mateso haya kama mbinu ya kuitumia kisiasa.

Kutaja majina na kuwatia aibu ndio mchezo uliopo, wanajionesha kama watesaji hivi leo ni jambo lenye kukarahisha, kama litawekwa wazi.

Na haya ni mafanikio makubwa ya mkataba wa kupinga utesaji, hali hii imesaidia kulileta suala hili la utesaji hadharani.

Wakati mataifa kadha tayari yameidhinisha mkataba huu, na kuna mataifa 51 ambayo bado hayajatia saini, ni dhahiri kuwa katika hali hii kunahitajika waraka wa ziada. Waraka huo wa ziada unaangalia udhibiti utakaofanywa na makundi huru katika jela , uchunguzi wa polisi pamoja na vituo vya makambi ya kuwazuilia watu kupitia vikundi vya kitaifa na kimataifa vya utawala.

Makundi haya yatathibitisha , iwapo mataifa hayo kwa kweli yenyewe binafsi yametia saini mikataba hiyo ya kutotumia mateso.

Nyaraka hizi za ziada hadi sasa zimetiwa saini na mataifa 33 tu. Kwa hali hii kuweza kufanyakazi itachukua pengine miaka mingine 20 ya kutumika mbinu ya kutaja majina na kuwatia aibu, hadi kuweza kuwa ni aibu kimataifa, kuwa katika kundi hilo la watesaji.

Maajabu ni kwamba , Ujerumani haimo katika mataifa yale yaliyotia saini waraka huo wa ziada, Marekani pia haijafanya hivyo.