1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafanikio ya sayansi.

Abdu Said Mtullya20 Julai 2009

Miaka 40 baada ya mwanadamu kutua mwezini.

https://p.dw.com/p/ItM3
Kamanda wa Apollo 11 Michael Collins.Picha: picture-alliance/ dpa/dpaweb

Miaka 40 iliyopita, mwanaanga wa Marekani, Neil Armstrong, alitua na kutembea mwezini, na hivyo kuwa mwanadamu wa kwanza kuchukua hatua hiyo.

Armstrong alisema wakati huo kuwa hatua aliyochukua yeye likuwa ndogo kwa mtu, lakini ilikuwa kubwa sana kwa binadamu wote.

Kwa kumpeleka mwanadamu mwezini, Marekani iliishinda Urusi katika mashindano ya kudhibiti anga za mbali.

Tarehe 20 mwezi Julai mwaka 1969 Chombo cha anga, Apollo 11, kiliwapeleka angani wanaanga watatu wa Marekani,Neil Armstrong, Buzz Aldrin na Michael Collins.Licha ya matatizo ya kompyuta yaliyokuwapo, chombo cha Eagle kilifanikiwa kutua mwezini. Wanaanga walikabiliwa na chaguo, kugeuza na kurudia au kuendesha mitambo kwa mikono yao. Walitumia mikono yao kuendesha mitambo.Armstrong alikuwa wa kwanza kuteremka na kutembea mwezini.

Watu zaidi ya nusu bilioni duniani kote walifuatilia tukio hilo kwenye televisheni miaka 40 iliyopita.

Mradi huo ulianza tarehe 25 mwezi Mei mnamo mwaka 1961 wakati rais John F. Kennedy aliposema " Marekani imechagua kwenda mwezini siyo kwa sababu ni rahisi kufaya hivyo, bali kwa sababu ni vigumu"

Huo ulikuwa wakati ambapo vita baridi baina ya Marekani na Urusi vilisthadi, na ambapo Urusi ilikuwa mbele katika utafiti wa anga. Wamarekani walinyongea.

Urusi ilikuwa ya kwanza kupeleka satelaiti angani na mwanaanga-Yuri Gagarin. Kutokana na hayo, Marekani ilipania kwa kila hali kumpeleka mwanadamu kwenye mwezi na ilifanikiwa.

Safari zingine tano zilifuatia. Kwa jumla, Wamarekani 12 wametua mwezini hadi sasa. Lakini shangwe zote zilitoweka haraka. Mmarekani wa mwisho kwenda mwezini alikuwa Eugene Cernon mnamo mwaka 1972. Baada ya hapo mradi wa Apollo ulimalizika.

Hata hivyo, wanaanga wa Marekani sasa wanatoa miito juu ya kutayarisha safari ya kwenda kwenye sayari ya Mars.

Mwandishi/Anna EngelkeMtullya, Abdu/ZR

Mhariri: Miraji Othman