1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 60 ya mfumo wa neema kwa wote

12 Juni 2008

Mfumo wa uchumi wa "neem,a kwa wote" nchini Ujerumani unaadhimisha miaka 60 Juni 20.2008.

https://p.dw.com/p/EIfd

Mfumo wa uchumi wa soko huru unaozingatia hali za wanyonge katika jamii-maarufu Ujerumani kwa jina la "Soziale Marktwirschaft", unaangaliwa ni mafanikio makubwa nchini Ujerumani baada ya vita vya pili vya dunia.

"Neema kwa wote" ndio tafsiri bora kabisa ya mfumo huu. Kiasi cha miaka 60 iliopita -yaani Juni 20, 1948,mfumo huu ulianza kwa mageuzi ya sarafu katika ile iliokua Ujerumani Magharibi.Haukua mwanzo usio na matatizo kinyume na wengi wanavyodhania hii leo.

►◄

Juni 20,1948 jiwe la msingi liliwekwa kuanzisha sarafu mpya .Miongoni mwa waasisi wake wa kile kilichoitwa "mageuzi ya sarafu" alikua mkurugenzi wa maswali ya uchumi katika zoni 3 za magharibi mwa Ujerumani na aliekuja baadae kuwa Kanzela wa Ujerumani:Ludwig Erhard.

"Baada ya kuumizana vichwa siku chache zilizopita,sasa hali zetu zimetulia .Wananchi wa Ujerumani wametulia na wameenda na shughuli zao.Na naamini si wengi miongoni mwao hawatakuwa na hisia kuwa ukombozi uliokuja umewanusuru chupu chupu kutumbukia shimoni."alisema Erhard.

Kile ambacho Kanzela Erhard amekusudia katika "kutumbukia shimoni " wajerumani walikiona baada ya kumalizika vita.Vitita vikubwa vya fedha walizokuwa nazo havikuwa na thamani yoyote.

Kwa Kanzela Ludwig Erhard mageuzi ya sarafu ilikua hatua ya kwanza kuelekea mfumo mpya wa kiuchumi uliozingatia pia hali za wanyonge katika jamii.Kitovu cha mfumo huo ni kuwapo uhuru wa kununua mtu atakacho na awezacho.Pawepo uhuru wa kufanya biashara,kuchagua kazi gani mtu apenda kufanya na kuchagua wapi angependa kutumika pamoja na haki ya kumiliki mali kibinafsi .Mapatano ya matajiri na vyama vya wafanyikazi kuafikiana ujira na mishahara bila kuingiliwa ni sehemu ya mfumo huo.

"Ni baada ya haki hizi kutimizwa katika hali ya uhuru wa kuchagua kazi na wapi kufanya kazi, uhuru wa kununua mtu atakacho,twaweza kutazamia kuwa wananchi wa Ujerumani wanachangia tena sehemu yao kuamua Ujerumani inafuata mkondo gani wa kisiasa na hatima yao."

Katika mfumo huu huru wa kiuchumi ,ilipangwa hasa taaasisi za kuwasaidia wanyonge katika jamii.Pawepo mfumo wa haki wa malipo ya kodi kwa kila mmoja na umilikaji mali usio na maonevu.

Awali Juni 20, ilikuwa ni siku ya mageuzi ya sarafu na madeni yote ya dola la Manazi yalifutwa.Mademni ya kibinafsi,mabaneki na akiba za fedha za watu binafsi zilithaminiwa kwa kipimo cha 1/10.Kila mkaazi wa maeneo ya magharibi mwa Ujerumani alipewsa DM 40 kama kianzio.

Ghafula ikabainika kana kwamba wajerumani wote ni matajiri sawa sawa na hakuna mwenye fedha zaidi.Ukweli lakini ulkikua vyengine kabisa.Mageuzi ya sarafu yaliwafaidia zaidi wale wenye hisa,waliomiliki majumba na viwanda.Sehemu kubwa ya umma walitoka mikono mitupu.Wale waliokuwa na akiba zao kwenye mabenki waliathirika mno.Kwani fedha zao zilibadilishwa kwa kipimo cha 100: 6.5Kutathmini mali zao kama ilivyodaiwa na vyama vya wafanyikazi hakujafanyika.

Mnamo siku za kwanza za ma