1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

150410 Papst Bilanz

Abdu Said Mtullya19 Aprili 2010

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 leo anatimiza mwaka wa tano tokea aanze kuliongoza kanisa katoliki.

https://p.dw.com/p/N05P
Baba Mtakatifu Benedikt wa 16.Picha: AP


Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 leo anatimiza mwaka wa tano tokea achaguliwe kuliongoza kanisa katoliki duniani. Aliingia katika wadhifa huo mwaka 2005 akiwa na lengo la kuimarisha umoja wa kanisa hilo.Jee amefanikiwa?

Kanisa katoliki limekumbwa na mikasa kadhaa katika kipindi hicho cha miaka mitano ya baba Mtakatifu Benedikt wa 16.Mikasa hiyo siyo tu kashfa ya kuharibiwa kwa watoto wa kiume na makasisi wa kanisa hilo.Kanisa katoliki lilitikiswa na mgogoro uliosababishwa na kasisi Williamson aliekana kutokea kwa maangamazi ya wayahudi. Katika kipindi hicho cha miaka mitano iliyopita hadhi ya kanisa katoliki imekuwa inatiwa dosari.

Leo katika maadhimisho ya miaka mitano katika uongozi wa kanisa katoliki watu wanauliza jee Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 analielekeza wapi kanisa?

Profesa wa maadili ya dini Eberhard Schockenhoff kutoka chuo kikuu cha Freiburg amejibu swali hilo kwa kueleza kwamba pamoja na mambo mengine pana mlolongo wa hatua za mashaka, kwa mtazamo wa kithiolojia. Profesa huyo amesema pana mashaka iwapo safari ya kanisa katoliki chini ya uongozi wa baba Mtakatifu Benedikt wa 16 litafikia shabaha ya kuwa kanisa lenye uwezo au iwapo msongamano wa mageuzi ulioanza kujikusanya miaka 30 iliyopita utashughulikiwa na baba mkatatifu huyo.

Katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wake baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amekuwa anapitia njia kati ya mdahalo na uhafidhina.

Katika mawaidha aliyoyatoa kwa makadinali miaka mitano iliyopita aliunga mkono njia ya mdahalo baina ya dini.Wengi walikuwa na matumaini ya kuona hatua za maendeleo. Lakini mkasa mwingine ulifuatia. Mhadhara alioutoa kwenye chuo kikuu cha Regensburg mnamo mwaka 2006 ulisababisha mzozo mkubwa na waislamu. Katika mhadhara huo baba Mtakatifu Benedikt wa 16 alimkariri mfalme wa kale aliesema kuwa dini ya kiislamu haukeleta chochote ilauovu tu!

Mnamo mwaka 2007 baba Mtakatifu huyo aliidhinisha hati iliyosababisha uhasama baina yake na kanisa la kiprotestanti!

Haikupita muda baba Mtakatifu alimrudisha katika usharika kasisi Williamson aliekana kutokea kwa maangamizi ya wayahudi wakati wa vita kuu vya pili.

Na sasa chini ya uongozi wake kanisa katoliki limekumbwa na kashfa kubwa. Siri juu ya kuharibiwa kwa watoto wa kiume na makasisi pamoja na kunyanyaswa kwa watoto hao zimekuwa zinafichuliwa mnamo siku za hivi karibuni.

Baada ya shinikizo kubwa kutoka kila upande baba Mtakatifu hatimaye amesema kuwa kanisa katoliki litachukua hatua za kuwalinda watoto, lakini pia litawachukulia hatua cha kisheria makasisi waliowafanyia watoto maovu.

Baba Mtakatifu Benediktwa 16 aliyatamka hayo katika ziara yake ya Malta.

"Kanisa linapaswa kuleta mambo mapya" Hayo ameyasema aliekuwa mwanafunzi wa baba Mtakatifu Beinert.

Mwandishi/Dechert Antje/ZA

Tafsiri/Mtullya Abdu/

Mhariri:Abdul-Rahman