1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya klombe la mataifa ya Ulaya

Mohammed AbdulRahman17 Oktoba 2007

Leo viwanja mbali mbali vya ulaya vitatimua tena vumbi katika michuano ya kandanda ya kusaka tiketi ya kucheza fainali ya kombe lijalo la mataifa ya Ulaya hapo mwakani nchini Austria na Uswisi.

https://p.dw.com/p/C7nL
Mshambuliaji wa Ujerumani Kevin Kuranyi akichukua mpira kwa kichwa ,katika pambano dhidi ya Ireland ambapo Ujerumani ilikata tiketi yake ya fainali za 2008.
Mshambuliaji wa Ujerumani Kevin Kuranyi akichukua mpira kwa kichwa ,katika pambano dhidi ya Ireland ambapo Ujerumani ilikata tiketi yake ya fainali za 2008.Picha: AP

Miongoni mwa makundi yanayoangaliwa kwa msisimko ni kundi B kati ya Scotland, Ufaransa na Italia.Scotland na Ufaransa zilizo katika kundi moja na pia England katika kundi E zote zinakabiliwa na majeruhi na adhabu ya kusimamishawa mechi za leo kwa baadhi ya wachezaji wao.

Scotland inayoongoza kundi B itamkosa Scott Brown aliyeumia pamoja na Alan Hutton na pia Lee McCulloch ambaye Gary Oconnor waliosimamishwa baada ya kupata kadi nyengine ya njano mechi iliopita, wakati Scotland ikichuana na Georgia mjini Tbilisi katika kiu chao cha kutaka kushiriki kaatika fainali za kombe la mataifa ya ulaya kwa mara ya kwanza tangu 1998.Scotland baada ya ushindi wa mabao 3-1 Jumamosi iliopita dhidi ya Ukraine sasa inahitaji pointi 4 tu kutokana na mechi mbili –ya leo na ile dhidi ya mabingwa wa dunia Italia mwezi ujao mjini Glasgow.

Ufaranasa ambayo pia iko kundi B ikiwa nyuma ya Itali katika nafasi ya tatu kawa tafauti ya pointi mbili dhidi ya Scotland na moja dhidi ya Italia , itaingia uwanjani leo bila ya mshambuliaji wake Nicolas Anelka anayesakata gozi katika timu ya ligi kuu ya England ya Bolton Wanderers na mlinzi Julien Escude anayechezea Sevilla ya Uhispania. Ufaransa inaikaribisha Lithuania mjini Nantes na itahitaji mchezo mwengine wa mashambulizi kama ilivyoshinda dhidi ya visiwa vya Faroe Jumamosi mabao 6-0.

Katika kundi E , England pia inakumbwa na majeruhi katika mchuano wake wa leo na Urusi mjini Mosko. Nahodha John Terrry na matatizo ya goti na Ashley Cole anasumbuliwa na kisigino. Nafasi ya Terry itajazwa na Sol Campbell.Baada ya ushindi wiki iliopita wa 3-0 dhidi ya Estonia, ushindi leo hii utaipa nafasi ya kwenda Austria na Uswisi na sare itawaacha wategemee matokeo ya mechi ijayo dhidi ya Kroatia inayoongotzwa kundi hilo, katika uwanja wa Wembley mwezi ujao.

Ureno nayo katika kundi la kwanza -kundi A itacheza ugenini na Kazakhstan wakati ikiwa na pointi 4 nyuma ya Poland inayoongoza kundi hilo na Ureno ina pointi sawa na Finland ambayo iko nafasi ya tatu, lakini Ureno ina mechi moja ya ziada kuliko Finland. Serbia timu nyengine katika kundi hilo ikiwa nyuma ya Finland inakaribishwa na Azerbaijan.

Utakumbuka msikilizaji Ujerumani imeshakata tiketi ya fainali hizo tangu Jumamosi ilipokwenda sare na Ireland bila kufungana mjini Durblin. Leo inamenyana na Jamhuri ya Cheki, ikiwa ni katika kukamilisha ratiba ya kundi hilo la D mjini Munich,.