1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miguna Miguna asema alileweshwa kabla ya kupelekwa Dubai

Iddi Ssessanga
29 Machi 2018

Mwansiasa wa upinzani nchini Kenya Miguna Miguna amedai kuwa alileweshwa na maafisa wa serikali kabla ya kusafirishwa hadi Dubai kwa nguvu, baada ya kukaa chooni alikozuiwa kwenye uwanja wa ndege kwa zaidi ya siku moja.

https://p.dw.com/p/2vBze
Kenia Anwalt und Oppositionspolitiker Miguna Miguna Nairobi
Miguna Miguna (mwenye kofia kushoto) akimuongoza Raila Odinga (katikati) kula kiapo kama "Rais wa wanachi" mwezi Januari). Kushoto ni James Orengo.Picha: Reuters/B. Ratner

Miguna Miguna, alielengwa katika ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Kenya kuhusiana na mzozo wa uchaguzi nchini humo, alipelekwa Dubai hata baada ya mahakama kuiziagiza mamlaka kumuachia, alisema wakili wake Cliff Ombeta.

Polisi katika uwanja wa ndege wa waliwafanyia vurugu mawakili na kuwalaazimisha kuondoka walipojaribu kuwakabidhi amri ya mahakama, alisema mwanasheria James Orengo.

Miguna alisema kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba maafisa walivunja mlango wa choo cha uwanja wa ndege ambako alikuwa ameshikiliwa na kumpiga sindano iliopmpelekea kupoteza fahamu. Alisema alipata tena fahamu wakati ndege ya shirika la Emirates ilipowasili Dubai.

Asema laazima arejee Kenya

Miguna aliandika kwamba anakataa kuondoka katika sehemu ya kimataifa ya uwanja wa ndege wa Dubai na anasisitiza kuwa laazima arejeshwe Kenya. "Nitarejea na laazima nirejee Kenya kama raia wa Kenya kwa kuzaliwa kama mahakama zilivyoagiza," aliandika Miguna kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kenia symbolische Vereidigung für Raila Odinga | Tom Kajwang, Miguna Miguna
Miguna Miguna akihudhuria hafla ya kujiapisha kwa Raila Januari 30 mjini Nairobi.Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Curtis

Hakukua na jibu la mara moja kutoka maafisa wa serikali ya Kenya, ingawa idara ya uhamiaji ya Kenya iliweka ujumbe kwenye  mtandao wa Twitter ikiutolea mwito umma kupuuza uvumi kwamba Miguna alitulizwa kwa dawa au kulishwa dawa za kulevya.

Kufukuzwa huko kulikomesha sarakasi zilizoshuhudiwa katika uwanja wa ndege wa Nairobi ambao Miguna aliweka ujumbe kutokea kile alichokiita "Choo katika kituo cha pili cha ndege", akisema alishikiliwa katika eneo chafu katika uwanja wa ndege wa taifa hilo.

Saa kadhaa kabla ya kusafirishwa, jaji wa mahakama kuu aliwatangaza waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, mkuu wa jeshi la polisi nchini humo na kamishna mkuu wa idara ya uhamiaji, kwa kudharau mahakama, kutokana na kupuuza amri ya kumuachia Miguna mara moja, alismea wakili Nelson Havi.

Jaji George Odunga aliamuru maafisa hao wafike mahakamani siku ya Alhamisi asubuhi au wafungwe jela. Miguna alifukuzwa na kupelekwa Canada mwezi uliopita katika ukandandamizaji dhidi ya wanasiasa waliohuduria hafla ya kujipisha kwa Raila Odinga kupinga kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta.

Baadae mahakama iliamuru kwamba hati ya Miguna ya kusafiria irejeshwe na kwamba aruhusiwe kurudi nchini. Hata hivyo, Miguna alipowasili siku ya Jumatatu katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, askari wa mwavuli walijaribu kumlaazimisha kupanda ndege inayoondoka, walisema mashuhuda. Hilo lilishindikana baada ya Miguna kupinga.

Kenia Präsident Uhuru Kenyatta und Oppositionsführer Raila Odinga in Nairobi
Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga walifikia muafaka kukomesha mzozo wa kisiasa nchini Kenya.Picha: Reuters/T. Mukoya

Makubaliano kati ya Uhuru na Raila

Makabiliano hayo ya uwanja wa ndege yalikuja wiki mbili baada ya mkutana kushtukiza kati ya kiongozi w aupinzani Raila Odinga na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, walipotangaza mpango mpya wa kutibu majeraha ya taifa hilo kufuatia miezi kadhaa ya vurugu za uchaguzi.

Odinga alihoji kwamba Kenyatta hakuwa na uhalali kwa sababu uhindi wake wa awali wa Agosti 8 ulibatilishwa na mahakama ya juu kuhusiana na kasoro na ukiukaji wa sheria. Uchaguzi wa marudio ulikuwa na uhudhuriaji mdogo baada ya Odinga kuususia, akidai magezi ya uchaguzi.

Miguna alikuwa upande wa Odinga wakati alipokula kiapo kama "rais wa wananchi" katika hafla hiyo ya kuigiza. Serikali ilijibu kwa kuendesha ukandamizaji dhidi ya wanasiasa wa upinzani.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/ape

Mhariri: Saumu Yusuf