Miguu, nyayo na kucha: Usanifu wa kipekee kwa viumbe hai
Leonardo da Vinci anauelezea mguu wa binaadamu kama "uumbaji wa kipekee." Miguu ya wanyama kwa hakika inavutia, maumbile yake tofauti tofauti yanayowawezesha walionayo kujiokoa, kukwea, kufukuza na mengine ya ziada.
Umepoteza kidole? Usihofu! Unaotesha tu kingine.
Axolotl, ambaye hufahamika pia kama samaki anayetembea, ni moja ya jamii ya mijusi wanaoshangaza duniani. Axolotls hawapitii hatua ya ukuaji iitwayo "Metamofosisi" (Mfano: kiwavi kwa kipepeo au ndubwi kwa vyura) ambayo ni kawaida kwa viumbe wengi wa jamii ya wadudu na Ampifibia. Wana uwezo mkubwa wa kuotesha tena viungo vyao na vidole vilivyokatika - ikiwa ni pamoja na miguu.
Mguu mdogo sana na mkubwa mkubwa sana
Mguu wa jamii ya panya buku wa kaskazini ya mji wa Luzon ukiwa pembeni ya mguu wa panya mdogo wa jamii ya Pygmy. Wanyama wote hao wanapatikana nchini Ufilipino. Kimsingi, kwa asili yao sio panya kamili bali ni jamii ya wanyama walao nyasi na waishio juu ya miti. Makaazi na tabia zao ni kama zile za vicheche. Na miguu yao ni imara sana kwa kukwea miti na kutimua mbio kukwepa wale wanaowawinda.
"Spiderman" — Kuwa makini na mwindaji huyu hatari!
Geckos ni aina ya mijusi wanaopatikana karibu kwenye kila bara duniani. Wanapenda kula wadudu na Buibui.Na huweza kutoka eneo moja hadi jingine kama "Spiderman" wakitumia miguu yao yenye asili ya kunatanata. Geckos wana vinyeweleo vidogo sana kwenye vidole vyao viitwavyo 'Setae'. Vinyweleo hivyo huiruhusu mijusi hiyo kuparamia hata maeneo yenye utelezi wa kutisha.
Yesu huenda alitembea juu ya maji, lakini 'Common Basilisk' wanaweza kukimbia.
Wakati mjusi huyu anapotimua mbio kukwepa wanaomuwinda hukusanya nguvu na mwendokasi wa kumwezesha kukimbia akitumia miguu yake ya nyuma. Common Basilisks wana miguu mikubwa ya nyuma na vidole vikavu. Wanaporuka majini huwa hujaa katikati ya vidole vyao. Kila wanapopiga hatua hewa hujaa tena baina ya vidole. Mijusi wadogo wa jamii hiyo huweza kukimbia juu ya maji kwa hadi mita 20.
Hakuna haja ya kukimbia
Buibui wa majini hawana sababu ya kutimua mbio ili kuelea majini kama ilivyo kwa Common Basilisks. Wao huelea tu. Nyayo zao zimetawaliwa na maelfu ya vinyweleo vidogo vidogo kama vile vya mjusi Gecko. Vinyweleo hivyo haviruhusu miguu isiingiwe maji. Buibui wa majini huwinda wadudu wadogo walio juu ya maji.
Mbuzi wapanda miti na vilima
Mbuzi ni viumbe vya kushangaza, kama ilivyo kwenye makazi ya vilima na theluji pia kwa jinsi wanavyokwea miti. Kwato zao za kipekee zinawapa uwezo wa kustahamili hata kwenye maeneo yenye mserereko katika viwambaza vya milima. Mbuzi wa milimani wanaweza kuruka katika eneo lenye mita chache tu. Wanatumia uwezo wao adimu kupanda juu kukwepa wanyama wanaowawinda ikiwemo dubu, simba na mbwa mwitu.
Ulimwengu wa kuuchapa usingizi kichwa chini miguu juu.
Popo wanaweza kuona wakiwa gizani wakitumia mfumo maalum uitwao "echolation". Wakiwa hawaruki, hutumia siku yao wakining'inia kichwa chini miguu juu kwenye maeneo yenye giza. Miguu yao imeumbwa mahsusi kwa ajili ya kukwea na kuning'inia katika maeneo ya miamba na misitu. Wakiwa kichwa chini miguu juu, uzito wao wa mwili hushikiliwa na nyanyo zilizofungwa zilizoshikilia barabara.
Unataka kujiunga nami?
Orangutans wanafahamika kwa vidole vyao virefu na vilivyojikunja. Kuwa na mikono minne kwa hakika ni bora kuliko kuwa na miwili. Miguu na mikono yao imeumbwa kwa kufanana mahsusi ili kupanda miti na kubembea. Orangutans wanaishi kwenye misitu ya mvua, zaidi katika maeneo ya juu ambayo wanayatumia kukwepa wanyama wanaowawinda.
Kwato za Farasi - Zaidi ya kitu cha kuwezesha kusimama.
Farasi kwa kawaida huwa na uzito wa kilo 400 hadi 900. Kwato zao huwasaidia kuhimili karibu asilimia 70 hadi 80 ya uzito na mwendokasi wa Farasi, ambao huweza kufikia Kilometa 88 kwa saa. Gamba gumu lililopo juu ya kwato hutoa ulinzi maridhawa kwa eneo laini la ndani ya kwato ambalo husaidia kupeleka damu miguuni na kuwezesha mzunguko wake.
Hebu niache kwanza - ninavaa viatu vyangu.
Jina lao kwa kilatini ni "miguu mia moja". Lakini licha ya jina hilo, Tandu huwa na idadi inayotofautiana ya miguu, kuanzia 30 hadi 354. Tandu ni kutoka kundi la viumbe wasio na uti wa mgongo. Hupatikana karibu kwenye kila bara duniani isipokuwa Antaktika. Miguu yao mingi huwasaidia kuishi gizani wakiitumia kama vipasha habari, vinavyowasaidia kuepuka kukwama kwenye maeneo finyu.
Kwenye barafu na mawimbi makali ? Ninaweza vyote viwili.
Penguins hawapatwi na baridi miguuni. Kama ilivyo kwa ndege wengine, wana sehemu lakini ya mishipa ya damu ambayo hufanya kazi ya kuipa joto miguu yao wakati wote. Miguu yao mipana hugeuka mapezi wanapoogelea. Ukijumuisha na maumbile yao mfano wa kombora, wanaweza kuzamia chini ya maji kati ya kilometa 10 hadi 20 ndani ya saa moja.