1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachunguzi wawili wa Umoja wa Mataifa wauwawa Congo

29 Machi 2017

Miili ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa raia wa Marekani na Sweden pamoja na mkalimani wao kutoka Kongo, imepatakana katika mkoa wa Kasai ya kati, watu hao walikuwa wakichunguza vurugu za karibuni nchini humo.

https://p.dw.com/p/2aDPP
Kongo Kananga Tshimbulu MONUSCO
Picha: Reuters/A. Ross

 " Baada ya kufanya  uchunguzi imegundulikana kuwa  miili hiyo  ni ile ya wachunguzi wawili wa Umoja wa Mataifa na mkalimani wao waliooneka katika mto Moyo," alisema msemaji wa serikali, Lambert Mende.

Msemaji huyo aliongezea kuwa wachunguzi wataendelea kuwatafuta wafanyakazi wengine   wakicongo waliopotea pia.

Michael Sharp kutoka Marekani, na Zaida Catalan kutoka Sweden, pamoja na mkalimani wao Betu Tshintela, na dereva Isaac Kabuayi pamoja na waendesha pikipiki wawili, walipotea tangu March 12 mwaka huu wakati walipokuwa wakifanya uchunguzi mkubwa juu ya vurugu na  ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na makundi ya majeshi nchini humo.

Inspekta wa polisi nchini Congo, Jenerali Charles Bisengimana, alisema kuwa miili hiyo ilionekana Jumatatu baina ya mji wa Tshimbula na Kanaga.

Baba wa Michael Sharp aliandika katika ukurusa wake wa  mtandao wa kijamii, facebook kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa miili iliyooneka inawezekana sana kuwa ya mwanawe na mfanyakazi mwenzake.

"Sikuweza kusema kitu, maneno yote yalinipotea, " aliaandika.

Guterres Aomboleza

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alisema kuwa uchunguzi utafanyika

ili kujua kitu gani kilitokea kwa wachunguzi hao wawili waliokufa. Mpaka sasa sababu ya

vifo vyao haijajulikana aliongozea kusema.

Guterres UN PK zu Hungersnöte in Afrika
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: picture-alliance/Zumapress/A. Lohr-Jones

"Michael na Zaida wamepoteza maisha yao wakati walipokuwa wakitaka kufahamu sababu zinazochangia kuwepo kwa vurugu na ukosefu wa usalama nchini Kongo, ili kuleta amani kwa nchi hiyo na wananchi wake," alisema Guterres wakati wa maombolezi.

Baadhi ya sehemu nchi Kongo, hususan upande wa mashariki, wamekuwa na vurugu na ukosefu wa usalama kwa muda mrefu sana , lakini pia vurugu limekuwepo pia katika sehemu ya jimbo la Kasai kati ya Congo.

Alipoulizwa kama  upoteaji wa wachunguzi na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, nchini Congo unaweza kuathiri Umoja wa Mataifa kutuma wataalamu nchi humo, naibu msemaji wa Guterres Farhan alisema kuwa  ana imani kuwa wataendelea kutuma wataalamu kufanya uchunguzi nchini humo, pale wanapohitajika. Aliongezea kusema pia kuwa bila shaka  hatua hiyo itachukuliwa kwa kuzingatia na kufahamu pia hali ya usalama nchi Congo.

Mwandishi: Najma Said

Mhariri :      Daniel Gakuba