1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miripuko yaitikisa Damascus

26 Septemba 2012

Waasi wa jeshi huru la Syria wamedai kuhusika na mashambulizi mawili ya bomu yaliyotokea leo katika majengo ya makao makuu ya jeshi la Syria katika mji mkuu Damascus. Watu kadhaa wameuawa.

https://p.dw.com/p/16EgS
epa03410574 A handout photo made available by Syria_s official news agency SANA shows columns of smoke rising from the site that has been hit by two powerful explosions in Damascus, Syria, 26 September 2012. According to media reports, two strong explosions rattled the upscale Abu Roumana neighborhood in the capital Damascus near the chief of staff_s offices and the aviation department and a fire broke out in the area. The area has witnessed heavy security presence and all roads leading to the site have been closed. EPA/SANA
Explosionen in DamaskusPicha: picture-alliance/dpa

Miripuko hiyo ililenga jengo la makao makuu ya jeshi katika uwanja wa Umayad katikati mwa Damascus. Hakukuwa na habari za haraka kuhusiana na idadi ya vifo wala majeruhi. Milio ya risasi na miripuko mingine midogo ilisikika mara baada ya mashambulizi hayo, pamoja na milio ya ving'ora vya magari ya kuwabeba wagonjwa. Barabara nyingi za kuelekea mjini humo zilifungwa.

Miripuko hiyo ilisikika mwendo wa saa moja asubuhi kabla ya watu kufika makazini. Shambulizi jingine la bomu mjini Damascus mnamo tarehe 18 Julai liliwauwa maafisa kadhaa wakuu wa usalama, akiwemo shemejiye rais Bashar al Assad, waziri wa ulinzi na mambo ya ndani. Shambulizi hilo liliwawezesha waasi kuingia ndani ya mji huo mkuu, ijapokuwa wamesukumwa nyuma hadi viungani.

Francois Hollande anapendekeza kulindwa maeneo ya makaazi Syria
Francois Hollande anapendekeza kulindwa maeneo ya makaazi SyriaPicha: dapd/AP

Wakati huo huo, Shirika la Kutetea Haki za Binadaamu la Syria limesema kuwa magenge ya wapiganaji wanayoiunga mkono serikali wamewauwa takribani raia 16 majumbani mwao mjini Damascus kabla ya mapambazuko leo. Mkuu wa shirika hil Rami Abdel Rahman amesema miongoni mwa waliouawa ni wanawake sita na watoto watatu.

Mgogoro wa Syria, ambao wakati mmoja ulikuwa tu wa maandamano ya amani, umegeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo Katribu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema ufumbuzi wake unahitajika haraka

Katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais wa Ufaransa Francois Hollande aliomba ulinzi wa Umoja wa Mataifa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi ili kusaidia kumaliza umwagaji damu na ukiukaji wa haki za binaadamu nchini Syria.

Naye rais wa Marekani Barack Obama aliishutumu Iran kwa kuunga mkono utawala wa kiimla nchini Syria. Obama alisisitiza kuwa utawala wa rais Assad ni lazima ufikie kikomo ili mateso na dhulma wanazopitia watu wa Syria ziishe na kuwekwe mustakabali mpya wa nchi hiyo.

Obama alisisitiza kuwa utawala wa kiimla wa rais Assad haufai kuendelea kuwa madarakani
Obama alisisitiza kuwa utawala wa kiimla wa rais Assad haufai kuendelea kuwa madarakaniPicha: Reuters

Katika hotuba nyingine kwenye mkutano huo, Mfalme wa Qatar Sheikh Hamad bin Khalifa al-Thani alisema nchi za magharibi ni lazima ziingilie kati nchini Syria kutokanana kushindwa kwa Baraza la Usalama kumaliza vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe. Alisema

Kuyalinda maeneo yatakayokombolewa yatahitaji amri ya kuzipiga marufuku ndege kuruka angani, ambayo inaweza kuzuia mashambulizi ya angani ya vikosi vya Assad dhidi ya maeneo yenye watu wengi.

Lakini hakuna dalili za hilo kufanywa na Baraza la Usalama kutokana na upinzani unaoendelea kutolewa na ura za turufu za Urusi na China. Marekani, washirika wa Ulaya, Uturuki na mataifa ya Ghuba ya Kiarabu yanaunga mkono upinzani Syria, huku Iran, Urusi na China zikimuunga mkono Assad.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters
Mhariri: Abdul-Rahman, Mohammed