1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miripuko yautakisa mji mkuu wa Libya

25 Julai 2011

Jumuiya ya kujihami ya NATO imetuhumiwa na serikali ya Libya kusababisha si chini ya vifo vya watu 7 na kuteketeza akiba ya chakula katika shambulio lililolenga mji wa Zliten,ulio mashariki ya mji mkuu wa Libya Tripoli.

https://p.dw.com/p/Rc2P
Anders Fogh Rasmussen, NATO Secretary General, speking at NATO MInisterial, Brussels, 8- 9 June, 2011. DW/Ani Ruci.
Katibu Mkuu wa NATO, Fogh RasmussenPicha: DW

Kundi la waandishi wa habari wa kigeni waliotembezwa katika mji huo ulio magharibi ya nchi, waliona jengo lililoteketezwa kabisa likiwa na nembo ya hilali katika lango la kuingilia uwanja wa kliniki ya kutibu magonjwa ya kuambukizana. Chupa za dawa na oxijeni zilikuwa zimetawanyika uwanjani lakini hawakuona wahanga wa shambulio hilo. Maripota hao walipelekwa katika eneo jingine la mji huo ambako walikuta majengo matatu ya kuhifadhi chakula yaliyoteketezwa kabisa na jengo moja lilikuwa likiwaka moto. Moshi ulikuwa ukivuka katika mamia ya magunia ya mchele, nyanya na mafuta ya kupikia, huku wazima moto wakihangaika kuudhibiti moto.

Waasi wa Libya wanaopigana tangu katikati ya mwezi wa Februari kwa azma ya kumuondosha madarakani kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, sasa wanaelekeza kampeni yao kwenye ngome ya Gaddafi mjini Tripoli. Lakini jitahada za kutaka kupitia mji wa Brega upande wa mashariki ya nchi zimekumbana na tatizo kubwa. Wanasema, mabomu yaliyofukiwa katika eneo linaloelekea Brega, ni tatizo lao kubwa kwani hawana vifaa vinavyohitajiwa kuondoa mitego hiyo.

In this image made from television, a dust cloud is seen following the explosion of a missile, outside the strategic oil port of Brega, Libya, Thursday, April 7, 2011. An apparent NATO airstrike slammed into a rebel combat convoy Thursday, killing at least five fighters and sharply boosting anger among anti-government forces after the second bungled mission in a week blamed on the military alliance. (AP Photo/National Transitional Council in Libya via AP Television News
Mripuko nje ya mji muhimu wa bandari BregaPicha: AP

Waasi hao, wanapigana na vikosi vya Gaddafi upande wa mashariki na wa kusini-magharibi, huku wakisaidiwa na ndege za jumuiya ya kujihami ya NATO. Lengo lao, ni kumaliza vita hivyo, kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanza tarehe mosi Agosti. Vita vya Libya vikichukua muda mrefu kuliko vile ilivyotazamiwa, nchi za magharibi sasa zinaimarisha jitahada za kidiplomasia, ili kupata njia ya kujitoa katika mgogoro huo.

Mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya amesema, mjumbe wa Umoja wa Mataifa atajaribu kuzishawishi pande mbili hasimu nchini Libya kuukubali mpango wa kumaliza vita na kuunda serikali ya kugawana madaraka, lakini bila ya Gaddafi. Msemaji wa serikali ya Libya, Mussa Ibrahim, amesema kuwa wajumbe wa Libya wapo tayari kuwa na majadiliano mengine pamoja na Marekani na waasi, lakini Gaddafi hatoondoka madarakani.

In this image taken from RTP Portugal TV, filmed in Tripoli, Libya, Thursday March 17, 2011, showing Libyan leader Moammar Gadhafi, during an interview as he comments on the prospects of a United Nations resolution against Libyan government forces. The interview made available Friday March 18, was filmed Thursday before the United Nations voted to authorize the use of "all necessary measures" to protect civilians under attack by government forces in Libya. (Foto:RTP Portugal TV/AP/dapd) TV OUT - PORTUGAL OUT - Mandatory credit RTP TV
Kiongozi wa Libya, Muammar GaddafiPicha: AP/RTP TV

Kwa upande mwingine, kundi la wanadiplomasia wa Libya na wafanyakazi walivamia ubalozi wa Libya katika mji mkuu wa Bulgaria, Sofia na wakatangaza kuwa ubalozi huo sasa unadhibitiwa na vikosi vya waasi wa Libya. Balozi mdogo Ibrahim al-Furis alieungana na waasi hao, amepewa muda wa saa 24 kuondoka Bulgaria. Wizara ya Mambo ya Nje ya Bulgaria imekataa kueleza sababu ya kuchukua hatua hiyo, lakini imesema kuwa haihusiki na kitendo cha kuuvamia ubalozi. Mwezi uliopita, Bulgaria ililitambua rasmi Baraza la Mpito la Taifa la waasi kama mwakilishi wa watu wa Libya.

Mwandishi:Martin,Prema/rtre,afpe

Mhariri:Yusuf Saumu