1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misaada zaidi kupambana na magonjwa

P.Martin28 Septemba 2007

Mfuko wa Dunia,kupambana na UKIMWI,kifua kikuu na malaria,utapokea kama Euro bilioni saba katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

https://p.dw.com/p/CH7X
Waziri wa Maendeleo Heidemarie Wieczorek-Zeul (kulia)na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani (kati)pamoja na mwenyekiti wa mkutano wa wafadhili wa Mfuko wa Dunia,Kofi Annan.
Waziri wa Maendeleo Heidemarie Wieczorek-Zeul (kulia)na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani (kati)pamoja na mwenyekiti wa mkutano wa wafadhili wa Mfuko wa Dunia,Kofi Annan.Picha: AP

Taarifa hiyo imetolewa na nchi 30 fadhili siku ya Alkhamisi katika mkutano wa Berlin.Ujerumani itachangia Euro milioni 600 hadi mwaka 2010.

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan,kama mwenyekiti wa mkutano wa mjini Berlin, amesifu mchango wa wafadhili.Amesema,malengo yaliyowekwa na jumuiya ya kimataifa ni hatua muhimu katika jitahada za kupambana na magonjwa duniani.

Hapo awali,Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,akiwa mwenyekiti wa sasa wa Kundi la Mataifa Manane Tajiri duniani- G8,alitoa wito wa kuwepo uratibu bora zaidi wa mipango ya afya.

Mfuko wa Dunia uliozinduliwa mwaka 2002 kwa jitahada za Kofi Annan,hadi hivi sasa umefanikiwa kuokoa maisha ya watu wapatao milioni 2.