1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yaufunga mpaka wake na Gaza

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1dT

Misri imeanza kuufunga mpaka wake na Gaza uliokikukwa siku 11 zilizopita wakati wanamgambo wa kundi la Hamas walipotengeneza njia na kuwaruhusu wapalestina wakimbie kutoka Ukanda wa Gaza kuingia Misri.

Maafisa wa usalama wa Misri wameanza kuvuka mpaka huo hii leo kuwazuia wapalestina wasivuke kuingia Misri. Maafisa hao wametumia nyaya za sing´eng´e na vizuizi vya chuma kukarabati sehemu ya mpaka iliyobomolewa.

Duru zinasema mamia ya maafisa wa usalama wa Misri wamepelekwa kushika doria katika mpaka kati ya Gaza na Misri.