1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mitazamo tafauti juu ya Muungano haijaigawa SMZ - Seif

15 Januari 2013

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amesema mitazamo tafauti miongoni mwa viongozi wa serikali juu ya hatima ya Zanzibar kwenye Muungano haijaigawa serikali hiyo yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.

https://p.dw.com/p/17KKW
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad.Picha: DW

Katika mahojiano maalum na Mohammed Khelef wa Deutsche Welle, kiongozi huyo anayeshikilia nafasi ya pili kwa umuhimu visiwani Zanzibar, amesema ni haki ya kila kiongozi kuwa na mtazamo wake kuhusiana na Muungano, na kwamba Serikali ya Zanzibar hadi sasa haina msimamo wake kuelekea suala hilo.

Kusikiliza mahojiano hayo, tafadhali bonyeza alama za spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Seif Sharif Hamad
Mhariri: Josephat Charo