1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miujiza ya wanawake uwanjani

11 Julai 2011

Timu ya taifa ya wanawake ya Marekani ilifufuka kutoka tofauti ya bao moja dhidi ya timu ya Brazil na pia kupungukiwa na mchezaji mmoja na kufanikiwa vivyo hivyo kuifunga timu hiyo kupitia mikwaju ya penalti.

https://p.dw.com/p/11tCY
Ni furaha na shangwePicha: dapd

Mabingwa hao wa michezo ya olimpiki walifanikiwa kulikomboa bao kunako sekunde kadhaa kabla ya kumalizika mechi hiyo baada ya kupata la kwanza kunako dakika mbili mwanzoni mwa mechi kufuatia Daiane wa Brazil kujifunga mwenyewe.

Frauen-Fußball-WM Viertelfinale 2011 Brasilien - USA
Daiane wa timu ya BrazilPicha: AP

Mchezaji nyota wa Brazil Marta aliifungia Brazil mabao 2 moja kupitia penalti.

Shukrani nyingi zimemuangukia Abby Wambach aliyesukuma hedi wavuni mwa Brazil na kusababisha mashabiki wa timu hiyo kushusha pumzi za afuweni, baada ya kukata tamaa ya timu hiyo kufuzu. Bao hilo liliweka mabao kati ya timu hizo mbili kuwa sare ya mabao 2-2 kufikia mwisho wa muda wa ziada.

Mikwaju ya penalti baadaye yaliipa timu hiyo ya Marekani ushindi dhidi ya Brazil baada ya kufanikiwa kuyatinga yote matano dhidi ya Brazil matatu.

Frauen-Fußball-WM Viertelfinale 2011 Brasilien - USA
Tobwe lake Abby Wambach wa MarekaniPicha: dapd

Marekani sasa inakabiliana na Ufaransa katika nusu fainali za mashindano hayo siku ya Jumatano baada ya wanawake wa Ufaransa nao kuwafunga Waingereza mikwaju 4 dhidi ya 3 ya penalti mjini Leverkusen, baada ya mechi hiyo pia kulazimika kuingia kiwango hicho cha Penalti baada ya timu hizo kumaliza kwa sare ya bao 1-1 mwishoni mwa muda wa ziada.

Uingereza ilikosa mara mbili katika kufunga penalti hizo huku Ufaransa ikipatiliza nafasi hiyo na hatimaye kufanikiwa kufuzu kwenye nusu fainali hizo.

Ufaransa iliudhibiti mpira wakati wote na ilikuwa na nafasi nyingi za kufunga kushinda wapinzani Waingereza.

Ama kwa upande wa mechi kuu kati ya Japan na mabingwa watetezi wa mashindano haya mwaka huu, Ujerumani, wanawake wa Japan waliyazima matumaini ya timu hiyo bingwa kulinyanyua kwa mara ya tatu mtawalia taji la mashindano hayo.

Flash-Galerie Frauen-Fußball-WM 2011 Viertelfinale Deutschland - Japan
Kerstin Garefrekes wa timu ya UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Karina Maruyama wa Japan alilifunga bao la pekee kunako dakika 108 kwenye mashindano hayo mjini Wolfsburg na kuwafungia Ujerumani mlango wa kuingia kwenye nusu fainali.

Ujerumani ilionekana kutamba katika awamu ya kwanza ya mechi hiyo lakini Japan ilianza kuchangamka baada ya saa moja ya mechi hiyo na iliwahangaisha wasichana wa kocha Silvia Neid kuanzia hapo hadi mwisho.

Japan ambayo iliofanikiwa kufika robo fainali pekee, mwisho mnamo mwaka 1995, itakutana sasa na Sweden ili kufuzu kwa fainali za mashindano haya mjini Frankfurt.

Frauen-Fußball-WM 2011 Viertelfinale Deutschland - Japan
Karina Maruyama na wenziwe wa JapanPicha: dapd

Sweden kwa upande wake iliishinda Australia mabao 3-1 mjini Augsburg.

Hii ni mara ya pili pekee ambapo timu ya Ujerumani imeshindwa kuwa mojawapo ya timu nne za mwisho katika mashindano haya ya kombe la dunia.

Kuumizwa pia kwa mchezaji Kim Kulig kunaonekana pia kubadilisha mpangilio wa mechi hiyo:

Mashindano haya yalikuwa ya mwisho kwa Kapteni Birgit Prinz ambaye anaondoka kwa hasira kufuatia kushindwa timu hiyo na vilevile hatua ya kocha wa timu hiyo kutomshirikisha katika mechi hiyo ya robo fainali na kwa kuikosa nafasi yake katika timu hiyo ya taifa katika mechi ya mwisho ya kikundi dhidi ya Ufaransa.

Prinz anaondoka kwenye soka ya kimataifa akiwa amefunga mabao 128 katika mechi 214 ikiwemo rekodi ya mabao 14 katika fainali za mashindano ya kombe la dunia. Alitarajia kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao katika ushindi mara tano wa mashindano hayo ya kombe la dunia, lakini ndoto hiyo haikuwa.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Dpae/Rtre/
Mhariri: Yusuf Saumu