1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjuwe Kansela Merkel

Zainab Aziz
24 Septemba 2017

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameshinda tena katika uchaguzi wa Jumapili tarehe 24 Septemba, akirejea mara ya nne madarakani. Lakini amewezaje kuufikia wadhifa huo muhimu wa kisiasa na sifa zake hasa ni zipi?

https://p.dw.com/p/2kGvq
CDU-Wahlkampf mit Angela Merkel
Picha: picture-alliance/dpa/F. Gentsch

Kansela Angela Merkel aliweka historia mara tu baada ya kuapishwa kuwa kansela mnamo mwezi Novemba mwaka 2005. hakuwa tu ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhfa huo wa Ukansela bali alikuwa ni kansela wa kwanza aliyetokea mashariki mwa Ujerumani eneo ambalo hadi mwaka 1990 lilikuwa linaongozwa kwa siasa za kisoshalisti.  

Tangu Merkel alipochukua madaraka, bila shaka ameweka alama ya sifa katika siasa za Ujerumani. Aliondoa hatua kwa hatua mpango wa nishati ya nyuklia, aliondoa sheria ya kuhudumu katika jeshi kwa lazima na alianzisha mafao kwa akina baba ambao hukaa nyumbani kwa muda mrefu ili kuwalea watoto wao, sera hizi zilimfanya apate uungwaji mkono kwa wingi hata kutoka kwenye vyama vya upinzani.

Deutschland Angela Merkel und Joachim Sauer
Kanselawa Ujerumani Angela Merkel na mumewe Joachim SauerPicha: picture-alliance/dpa/T. Hase

Kansela Merkel pia ni kiongozi anayeheshimiwa katika bara Ulaya na kwingineko. Mnamo 2016, gaueti la Marekani la New York Times ililimtaja bi Merkel kuwa ni mmoja wa watetezi wa uhuru waliobakia ulimwenguni. Merkel aliongoza mjadala kati ya viongozi wa Ulaya wakati wa mgogoro wa sarafu ya Euro wa mwaka 2010.

Kansela Angela Merkel alipendekeza hatua kali kwa ajili ya kuziokoa nchi kama vile Ugiriki ili zisifilisike. Wakosoaji walisema hatua hizo zimesababisha umasikini na ukosefu wa ajira. Mwaka 2015, Bi Merkel aliwashangaza Wajerumani wengi na majirani zake katika nchi za Ulaya pale alipofungua mipaka ya Ujerumani kwa wahamiaji karibu 900,000 kutoka Syria, Afghanistan na mahali pengine.

Wakosoaji wa Bibi Merkel wanalalamika kwamba alishindwa kutekeleza mageuzi katika ya sekta ya afya na katika mfumo wa pensheni ili kuepuka hasira ya umma. Wanasema pia Merkel anabadili misimamo yake ya kisiasa kwa haraka ili aendelee kuwa maarufu. Kwa mfano, Bi Merkel wakati mmoja alikuwa anaunga mkono matumizi ya nishati ya atomiki. Baada ya ajali kwenye kinu cha nyuklia cha Fukushima huko Japan mnamo mwaka 2011 akageuka na kusema kuwa ni muhimu kukifunga.

Binz Wahlkampf CDU - Merkel
Mwanaume akiwa na bango linalosema kansela Angela Merkel aondoke.Picha: Reuters/A. Schmidt

Mpinzani wake mkuu katika uchaguzi wa mwaka huu Martin Schulz,amemlaumu mara kwa mara kwa kuepuka mijadala wa umma na kueleza wazi misimamo yake. 

Bi Merkel ameahidi kutumikia muda kamili wa miaka minne kama kansela iwapo chama chake kitashinda  katika uchaguzi wa Jumapili tarehe 24 mwezi Septemba mwaka huu wa 2017. Nafasi hiyo itaweza kumfanya kuwa kansela wa pili atayehudumu kwa kipindi kirefu tangu kumalizika Vita Kuu ya pili.


Mwandishi: Zainab Aziz/Daniel Pelz

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman