1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa haki za msingi Ulaya

12 Desemba 2007

Kesho viongozi wa dola na serikali wa Umoja wa Ulaya watatia saini mkataba wa haki za msingi.

https://p.dw.com/p/Calh

Inasikika vizuri, lakini katiba ya haki za kimsingi ya umoja wa Ulaya , ina manufaa gani kwa wakaazi wake ?

Maoni hapo yanatofautiana.Katiba hii ya haki za msingi ya UU kwa mara nyengine inatangazwa leo rasmi katika sherehe maalumu huko Strassbourg,makao makuu ya Bunge la ulaya.

Kesho alhamisi viongozi wa dola na serikali watatia saini zao:

Miaka 7 iliopita wakati wa mkutano wa kilele wa Nice,Ufaransa, mkataba wa haki za kimsingi katika Umoja wa Ulaya ulifungwa .Wakati ule ulipotangazwa haukuanza kutumika kisheria.Hivi sasa lakini kupitia mkataba uliofanyiwa maguezi wa katiba ya Ulaya utweza kuanza kazi.Mkataba huu ambao awali uliitwa katiba ya UU utatiwa saini hapo kesho alhamisi na viongozi wa dola na serikali na utaweza kuanza kazi mnamo miaka 2 ijayo.

Hapo tena mkataba huo wa haki za kimsingi utaegemea sheria .

Kimsingi mkataba huo unampa raia katika Umoja wa Ulaya unaozidi kupanuka ,ulinzi wa haki zake ili kujitetea na maamuzi yanayoamuliwa Ulaya kisiasa.

Kanzela Angela Merkel, hapo juni, mwaka huu mwishoni mwa wadhifa wake kama rais wa UU amepongeza mkataba huo.

Alisema ,

„Kwa mkataba wa haki za msingi ,haki za raia wake wak waume zitaimarika.Mkataba wa haki za kimsingi unaegemea sasa sheria ambao kwa jicho langu unastahiki Ulaya iliokomaa.“

Sehemu kubwa ya haki hizo za kimsingi zimo nda ni ya katiba za nchi mbali mbali zanachama-kwa mfano utu wa mwanadamu uheshimiwe na kwamba hakuna anaestahiki kubaguliwa tangu kijinsia au kwa rangi yake .Katiba ya msingi ya UU inalenga kutoa hata haki zaidi.Kila raia kwa mfano ana haki kutafuta na kupata kazi popote pale alipo barani Ulaya au kutumika katika huduma za nchi hizo.

Mkataba huu unahkikisha pia haki za kimsingi za kufanya kazi za utu wa kibinadamu na sio kiutumwa na kufungua milango ya elimu pamoja na ulinzi wa taarifa za mtu binafsi-hii ikiwa ni mifano fulani tu.

Endapo raia yeyote akihisi ametendewa si haki katika nchi moja na vyombo vya dola au vya kisheria ana haki kupeleka kesi yake katika mahkama za Ulaya huko Luxembourg.

Ili kuzima mlongo wa mashtaka ,itampasa kwanza mtu kupitia mahkama za kitaifa kabla ya kwanza kupeleka mashtaka yake Ulaya.

Kimsingi lakini mahkama za kitaifa na sheria za kitaifa pamoja na katiba ya kitaifa ndio muongozo wa kmila raia kuegemea.Na kwa nchi kama Uingereza na Poland ,mkataba huo wa haki za kimsingi hautawahusua raia wake alao kwa sasa.Hasa Uingereza inahofia wafanyikazi wake kulalamika katika mahkama kuu ya ulaya juu ya haki zao za kazi.