1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa Mageuzi wa Umoja Ulaya kusainiwa leo

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbCU

LISBON

Viongozi wa Umoja wa Ulaya leo hii wanatazamiwa kukutana katika mji mkuu wa Ureno Lisbon kutia saini Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya.

Mkataba huo utachukuwa nafasi ya katiba ya Umoja wa Ulaya ilioundwa awali ambayo ilikataliwa na wapiga kura wa Uholanzi na Ufaransa hapo mwaka 2005.Mkataba huo unakusudia kuzifanya taasisi za umoja huo kuwa za kisasa na kuufanya umoja huo kuwa na demokrasia zaidi.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akizungumza kwenye bunge la Ujerumani ameuita mkataba huo kuwa ni msingi wa Umoja mpya wa Ulaya katika karne ya 21.

Hata hivyo mkataba huo hautoanza kutumika hadi hapo nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya zitakapouridhia.Mchakato wa kuridhiwa iwapo utakamilishwa na mapema itakuwa ni mwaka 2009 wakati wa uchaguzi mpya wa Ulaya.