1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mke wa mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani awekwa kizuizini

11 Oktoba 2010

Mke wa mshindi wa mwaka huu wa Tunzo ya Amani ya Nobel Liu Xiaobo, Bibi Liu Xia, amezuiliwa nyumbani kwake mjini Beijing na vyombo vya usalama vya Serikali ya China

https://p.dw.com/p/PasP
Mke wa mshindi wa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2010, Liu Xiaobo, Bibi Liu Xia
Mke wa mshindi wa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2010, Liu Xiaobo, Bibi Liu XiaPicha: Mathias Bölinger

Msemaji wa Shirika la haki za binadamu la Marekani lenye makaazi yake nchini China, amesema Bibi Liu Xia amewekwa katika kizuizi cha nyumbani.

Alikuwa amekwenda kumtembelea mume wake gerezani ili kumpa habari za ushindi wa tuzo ya amani na kwamba aliporudi nyumbani kwake mjini Beijing alizuiwa asitoke.

Liu Xiaobo, mshindi wa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka wa 2010
Liu Xiaobo, mshindi wa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka wa 2010

Liu Xiaobo alishinda tuzo ya amani ya Nobel siku ya Ijumaa kutokana na miongo miwili ya harakati zake zisizotumia nguvu ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa nchini China.

Mwandishi: Halima Nyanza(ZPR)

Mhariri: Sekione Kitojo