1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutanao wa 21 wa kilele kati ya China na Umoja wa Ulaya

Oumilkheir Hamidou
9 Aprili 2019

Waziri mkuu wa China Li Keqiang atakutana na viongozi wa Umoja wa ulaya mjini Brussels kuzungumzia mada tete ikiwa ni pamoja na kuakilishwa kwa upana zaidi makampuni ya Ulaya katika masoko ya China na haki za binaadam

https://p.dw.com/p/3GUqu
Peking EU China Treffen Tusk Li Keqiang Juncker
Picha: Reuters/T. Peter

Kwa mujibu wa wadadisi, majadiliano magumu yanatarajiwa kugubika mkutano huo wa kilele kati ya waziri mkuu wa China Li Keqiang na viongozi wa Umoja wa ulaya mjini Brussels. Kinyume na mkutano wa kilele kati ya China na viongozi wa Afrika septemba mwaka 2018 ambapo televisheni ya nchi hiyo ilizungumzia kuhusu "mkutano wa familia", ndoto za pamoja na urafiki wa kudumu". Kwa sababu licha ya miezi kadhaa ya maandalizi, Umoja wa ulaya hautopata hii leo  yale inayodhamiria kuyapata kutoka China: Na mambo hayo ni pamoja na kuheshimiwa haki za binaadam, biashara ya haki na uwezekano wa kuwekeza.

Waziri mkuu wa China akitoa wito wa kuchukuliwa hatua kukabiliana na matatizo yaliyozushwa na wafanyabiashara wa Umojan wa Ulaya katika mkutano wa kilele wa mwaka 2018
Waziri mkuu wa China akitoa wito wa kuchukuliwa hatua kukabiliana na matatizo yaliyozushwa na wafanyabiashara wa Umojan wa Ulaya katika mkutano wa kilele wa mwaka 2018Picha: Getty Images/N. Guan

Taarifa ya mwisho haitarajiwi kuchapishwa

Mtaalam wa masuala ya China kutoka taasisi ya Mercantor ya taaluma za China mjini Berlin, Mikko Huotari anasema:"Matarajio ni finyu. Kuna hali jumla inayojitokeza katika mkutano kama huu wa kilele pamoja na China, huwezi kuashiria mapema matokeo yatakuwa ya aina gani. Na yadhihirika kana kwamba uwezekano ni mkubwa hata taarifa ya pamoja haitotolewa mwishoni mwa mkutano."

Ingawa mada mfano wa mabadiliko ya tabianchi, siasa ya nje na usalama mtandaoni zinatarajiwa kujadiliwa, lakini kipa umbele katika mkutano huu wa 21 wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na China ni kuhakikisha " watu wanatendeana sawa katika shughuli za biashara na uwekezaji."Inamaanisha ikiwa makampuni ya China yanafaidika na masoko wazi ya Ulaya, hali iwe vivyo hivyo kwa makampuni ya Ulaya nchini China.

Mkutano wa kilele wa China na Umoja wa Ulaya ulioitishwa mwaka 2018 mjini Brussels
Mkutano wa kilele wa China na Umoja wa Ulaya ulioitishwa mwaka 2018 mjini BrusselsPicha: picture-alliance/AP Photo/N. Han Guan

Haki za binaadam bado ni mwiba wa mchongoma katika uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya

Ndio maana Umoja wa ulaya unajadiliana na China kuhusu makubaliano ya kulinda vitega uchumi. Pindi mazungumzo yakiendelea vyema, makubaliano hayo yatakamilishwa mwakani, amesema hayo waziri wa Romania anaeshughulikia masuala ya Umoja wa Ulaya Gabriela Ciot.

Ka mujibu wa mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya, China na Umoja wa Ulaya hawakubaliani bado kuhusu suala la haki za binaadam. Pembezoni mwa mkutano wa kilele, kuna majadiliano yanayoendelea kuhusu mada hiyo majadiliano ambayo Mikko Huotari wa taasisi ya Mercantor anayaangalia kama kipimo cha mazungumzo yatakayofuatia.

 

Mwandishi: Gohr,Lara/Hamidou Oummilkheir