1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kati ya Erdogan na Merkel Berlin

31 Oktoba 2012

Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan na Kansela wa ujerumani Angela Merkel wanakutana mjini Berlin huku suala kuu likiwa ni hali nchini Syria. Uturuki inawahifadhi wakimbizi laki moja wa Syria.

https://p.dw.com/p/16Zs0
German Chancellor Angela Merkel, right, and Turkey's Prime Minister Recep Tayyip Erdogan, left, address the media during a news conference after a meeting at the Chancellery in Berlin, Germany, Wednesday, Nov. 2, 2011. (Foto:Michael Sohn/AP/dapd)
Deutschland Türkei Festakt zu 50 Jahre deutsch-türkisches Anwerbeabkommen Recep Tayyip ErdoganPicha: dapd

Huku mgogoro wa Syria wakati mwingine ukivuka hadi Uturuki, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle aliisifu serikali ya nchi hiyo kuhusu namna inavyolishughulikia suala hilo. Alisema wao kama washirika wa Jumuiya ya NATO, Ujerumani inasimama na Uturuki. Aliyesasema hayo wakati alipokutana na Waziri Erdogan mjini Berlin, ambaye leo anafanya mazungumzo na Kansela wa Merkel.

Westerwelle alitoa wito wa kuanzishwa upya mazungumzo ya kuijumuisha Uturuki katika Umoja wa Ulaya, ambayo yalikwama tangu mwaka wa 2005, kutokana na mgogoro wa muda mrefu baina ya Uturuki na mwanachama wa umoja huo Cyprus. Westerwelle amesema kuwa mkwamo huo wa miaka miwili katika mazungumzo hayo haujakuwa mzuri kwa pande zote husika.

Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amezindua rasmi ubalozi wa nchi hiyo Ujerumani
Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amezindua rasmi ubalozi wa nchi hiyo UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Wakati chama cha Westerwelle cha Free Democratic Party kikiunga mkono uwanachama wa Uturuki katika Umoja wa Ulaya, chama chake Kansela Angela Merkel cha Christian Democratic Union kinapinga.

Wakati Uturuki na Ujerumani zikiwa na uhusiano dhabiti wa kibiashara, uhusiano baina ya nchi hizo mbili wakati mwingine umeathirika kutokana na namna Ujerumani inavyowashughulikia wahamiaji kutoka Uturuki, pamoja na shutuma za Ujerumani kuhusu namna nchi hiyo inavyowashughulikia raia wake wa Kikurdi walio wachache.

Takriban watu milioni 2 na nusu wanaoishi Ujerumani wana asili ya Kituruki, na Erdogan amewaomba kuzungumza vyema Kijerumani pamoja na Kituruki, ili waweze kutangamana vyema katika taifa lao mwenyeji.

Akizungumza jana, Waziri huyo mkuu wa Uturuki alisema kwama Umoja wa Ulaya utaipoteza Uturuki kama hautaipa uwanachama ifikapo mwaka wa 2023. Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Erdogan kudokeza kuhusu muda ambao Uturuki huenda ikaendelea kuwa nao katika juhudi za kujiunga na Umoja wa Ulaya. Wakati huo Uturuki itakuwa ikiadhimisha miaka 100 ya uanzilishi wake kuwa Jamhuri kutoka kwa utawala wa Ufalme wa Ottoman.

Jengo la ubalozi mpya wa Uturuki mjini Berlin, Ujerumani
Jengo la ubalozi mpya wa Uturuki mjini Berlin, UjerumaniPicha: AFP/Getty Images

Erdogan alisema Uturuki ambayo ina jumla ya idadi ya watu milioni 74 wengi wao Waislamu itauongezea nguvu Umoja wa Ulaya. Takribani Waturuki milioni sita tayari wanaishi katika nchi za Umoja wa Ulaya, na takribani milioni tatu kati yao wanaishi Ujerumani.

Uturuki imekamilisha kifungu kimoja tu kati ya 35 vya sera ambavyo kila nchi inayotaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya lazima ikamilishe. Vifungu vyote vya sera isipokuwa 13 pekee katika mazungumzo ya Uturuki vinapingwa, na Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, ambayo ni mkono wa utendaji wa Umoja wa Ulaya, inasema Uturuki bado haitimizi viwango vinavyohitajika kuhusu haki za binaadamu na uhuru wa kujieleza

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters

Mhariri: Daniel Gakuba