1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kati ya Ujerumani na Urusi

19 Julai 2011

Rais wa Urusi, Dmitr Medvedev amekutana na Kansela Angela Merkel mjini Hannover Ujerumani kwa kikao cha pande mbili cha siku mbili

https://p.dw.com/p/11zBJ
Rais wa Urusi Dmitr Medvedev na Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: picture alliance/dpa

Rais wa Urisi Dmitr Medvedev amewasili nchini Ujerumani hapo jana kwa mazungumzo na Kansela Angela Merkel.

Deutsch-russische Regierungskonsultationen: Merkel und Medwedew
Ni mkutano unaofanyika kila mwaka kati ya nchi hizo mbiliPicha: AP

Viongozi hao wanakutana katika mji uliopo kaskazini, Hanover, kwa kikao cha pande mbili cha siku mbili. Ni mkutano wa 13 wa kila mwaka wa viongozi wa kisiasa na kibiashara kutoka nchi hizo mbili.

Huenda uhusiano unaokuwa wa kibiashara kati ya Ujerumani na Urusi ndio ukatawala kikao hicho. Ujerumani ni mshirika wa kipekee wa muhimu kibiashara kwa Urusi ,na Urusi ni muuzaji mkubwa wa nje wa nishati kwa Ujerumani.

Mwandishi:Maryam Abdalla/afp, dapd

Mhariri:Kitojo Sekione